Kushughulikia masuala ya faragha na
usalama katika uhandisi jijini Munich.

GSEC Munich ni kitovu cha kimataifa cha Google kilicho na wahandisi wanaoshughulikia masuala ya faragha na usalama, kinachopatikana katikati mwa bara la Ulaya. Kituo hiki kilianzishwa mwaka 2019 na kina zaidi ya wahandisi 300 wenye bidii ambao hujitahidi kubuni bidhaa na zana ambazo zitasaidia kulinda usalama wa kila mtu mtandaoni na kuhifadhi taarifa zake kwa faragha na usalama.

Kuangazia mikakati ya GSEC Munich.

GSEC Munich hubuni bidhaa na zana ambazo husaidia kulinda usalama wa mamilioni ya watu mtandaoni. Vidhibiti hivi ambavyo ni rahisi kutumia, ulinzi uliojumuishwa kwenye mfumo na teknolojia za programu huria zimebuniwa ili kutoa huduma bora zaidi ya faragha na usalama kwa kila mtu.

KIDHIBITI CHA NENOSIRI

Njia salama zaidi ya kudhibiti manenosiri yako

Kidhibiti chetu cha Nenosiri, ambacho kimejumuishwa moja kwa moja katika Chrome, Android na Chrome kwenye iOS, ni njia salama zaidi ya kulinda akaunti zako zote mtandaoni. Manenosiri yako yaliyohifadhiwa hulindwa kila wakati kupitia ulinzi wa kiotomatiki wa Google na tutakufahamisha tukibaini kuwa tovuti au programu ambayo umehifadhi nenosiri lake imeathiriwa. Pia, unapojisajili kwenye programu au tovuti mpya, Kidhibiti cha Nenosiri kinaweza kutunga kiotomatiki nenosiri la kipekee na changamani, ambalo huwekwa kiotomatiki utakapoingia kwenye akaunti wakati ujao.

Kutana na watu
wanaofanikisha GSEC Munich.

GSEC Munich ina zaidi ya wahandisi 300 walioko jijini Munich lakini wanatoka Ujerumani na nchi zingine. Wahandisi hawa hujitahidi kubuni intaneti salama zaidi kwa ajili ya ulimwengu wote.

Picha ya Werner Unterhofer

"Tunahakikisha watumiaji wanaweza kuchagua kiwango cha ukusanyaji wa data ambacho wanahisi kinawafaa – na kuwapa zana za kufuta data endapo watapenda kufanya hivyo."

Werner Unterhofer

TECHNICAL PROGRAM MANAGER
Jan-Philipp Weber

"Masuala ya faragha na usalama huwa muhimu na ni ya kibinafsi sana; yote mawili yanapaswa kutimizwa kwa urahisi."

Jan-Philipp Weber

SOFTWARE ENGINEER
Elyse Bellamy

"Tunalenga kuwapa watumiaji vidhibiti ili kubaini data ambayo wangependa kushiriki na Google na kuchagua muda ambao wanahisi data hiyo inafaa. Usanifu wa kukisia hurahisishia watumiaji mchakato wa kupata, kutumia na kudhibiti data na mapendeleo yao ya faragha."

Elyse Bellamy

INTERACTION DESIGNER
Jochen Eisinger

"Tungependa watumiaji wadhibiti faragha na usalama wao mtandaoni bila wasiwasi wowote. Watumiaji wanataka kuvinjari intaneti na tunahitaji kuwapa mipangilio chaguomsingi iliyo salama na adilifu wanapofanya hivyo."

Jochen Eisinger

DIRECTOR OF ENGINEERING
Audrey An

"Kila mtu ana haki ya faragha bila kujali nyenzo au ujuzi wa kiufundi. Lengo letu ni kubuni zana zinazomwezesha kila mtu achague kinachomfaa na anachofanya wakati mahususi."

Audrey An

PRODUCT MANAGER
Sabine Borsay

"Watu wanapaswa kuvinjari intaneti kwa usalama, wakihisi kuwa wanaweza kudhibiti hali yao ya utumiaji. Ulinzi chaguomsingi ambao ni thabiti na mipangilio iliyo rahisi kutumia ya faragha na usalama ni vigezo muhimu vya ulinzi wa mtumiaji mtandaoni na lengo letu la kila siku."

Sabine Borsay

PRODUCT MANAGER
Nyuma ya pazia
katika Kituo cha Uhandisi wa Usalama kwenye Google.

Tunaongea na watumiaji duniani kote kuelewa maswala yao kuhusu usalama wa Intaneti. Tunapatia timu ya wahandusi wetu nafasi, msukumo na usaidizi kutengeneza suluhu za kizazi kijacho kusaidia kuimarisha usalama mtandaoni.

Uboreshaji wa usalama mtandaoni

Pata maelezo kuhusu jinsi tunavyohakikisha usalama wa watu wengi zaidi mtandaoni kuliko mtu mwingine yeyote duniani.