Kila siku Google hufanya kazi kuhakikisha kuwa intaneti ni salama kwa kila mtu

Angalia michango yetu
Mbinu zetu

Kulinda watu, biashara na serikali

Usalama ni nguzo ya mkakati wetu wa bidhaa. Ndio maana bidhaa zetu zote zina ulinzi uliojumuishwa ambao unafanya ziwe salama kwa chaguomsingi.

Pata maelezo zaidi

Kuiwezesha jamii kushughulikia hatari za usalama mtandaoni

Tunaiwezesha jamii kutumia uwezo wa programu huria na kushiriki maarifa na utaalamu wetu na sekta kwa uwazi ili kuifanya mifumo iwe salama.

Pata maelezo zaidi

Boresha teknolojia za siku zijazo

Tunataka kulinda jamii dhidi ya kizazi kijacho cha vitisho vya mtandaoni. Kuimarisha utaalamu wetu wa AI, tunabuni awamu ijayo ya usanifu utakaovuka mipaka ya ubunifu wa usalama.

Pata maelezo zaidi
Linda watu, biashara na serikali

Tunabuni ulinzi ulioboreshwa katika kila hatua ya uundaji wetu wa bidhaa na miundombinu ya wingu. Hatua hii inawezesha mashirika kuwa ya kisasa na kuimarisha ulinzi wao wa TEHAMA huku wakisaidia watumiaji kulinda taarifa zao binafsi na kufikia Intaneti kwa usalama.

Wezesha jamii kushughulikia hatari za usalama mtandaoni

Tunashirikiana na viongozi wa usalama mtandaoni, serikali na jumuiya za usalama ili kuboresha viwango vya kimataifa vinavyotoa kipaumbele kwa ulinzi wa mtumiaji, vinapambana na taarifa za kupotosha na kushiriki taarifa za vitisho ili kuifanya Intaneti iwe wazi na salama kwa kila mtu.

Boresha teknolojia za siku zijazo

Tunashughulikia kuhakikisha usalama wa watumiaji walio kwenye hatari ya kushambuliwa mtandaoni huku tukilinda faragha yao kupitia maboresho ya AI, maunzi, matumizi ya kompyuta kwenye wingu na kuweka viwango vya kimataifa vya matumizi ya kompyuta kwa njia ya kwanta.

Ushirikiano ili kuifanya intaneti iwe salama zaidi kwa kila mtu

Usalama wa mtandaoni ni shughuli ya kushirikiana, na tunapofanya kazi pamoja, tunaweza kuchochea ubunifu na kubuni mbinu bora zinazowanufaisha wote kwenye mazingira haya magumu, yanayobadilika mara kwa mara.

Bango la Kituo cha Uhandisi wa Usalama kwenye Google nje ya ghorofa refu.
Vituo vya Usalama na Uhandisi kwenye Google

Timu zetu zinafanya kazi katika nyanja za faragha, usalama, uwajibikaji wa maudhui na usalama wa familia kote duniani. Kituo chetu cha Uhandisi wa Usalama kwenye Google kinasaidia kuongoza kazi hii, inayoongozwa na wahandisi, wataalamu wa sera na maudhui wenye uzoefu.

Onyesho la kukagua la ukurasa wa kwanza wa Google Bug Hunters likionyesha kolagi ya ishara za wasanidi.
Google Bug Hunters

Jumuiya yetu ya kimataifa ya Bug Hunters inatathmini kwa kina bidhaa zetu ili kuzifanya ziendelee kufanya kazi kwa namna inayotakiwa na kufanya intaneti kuwa mahali salama zaidi.

Wataalamu watatu wakishirikiana mbele ya kompyuta, huku mmoja akiwaonyesha wenzake wawili usalama mtandaoni.
Timu ya Kazi ya Usalama Mtandaoni ya Google

Tunatumia timu bora zaidi ya ushauri wa ulinzi ili kutegemeza mabadiliko ya dijitali na usalama ya serikali, miundombinu muhimu, biashara na biashara ndogo ndogo.

Gundua mbinu nyingi tunazotumia
kuimarisha usalama wako mtandaoni.