Matangazo ambayo yanaheshimu faragha yako.

"Hakuna kilicho muhimu zaidi ya kudumisha usalama wako mtandaoni. Kubuni bidhaa zilizo salama kwa chaguomsingi, zinazozingatia faragha na zinazokupa udhibiti, ndivyo tunavyohakikisha kuwa, kila siku, uko salama zaidi kwenye Google.”

- Jen Fitzpatrick, Makamu wa Rais Mwandamizi, kitengo cha Mifumo ya Msingi na Matumizi katika Google

Kujitolea kwetu kuonyesha matangazo kwa kuwajibika.

Kudumisha mtandao kuwa wazi, wa faragha na salama, ni jambo la msingi tunalofanya. Tumejitolea kutoa matangazo kwa kuwajibika. Ifuatayo ni jinsi kanuni za faragha za Google zinavyotumika kwenye matangazo:

Kamwe hatuuzi taarifa zako binafsi kwa mtu yeyote.

Kamwe hatuuzi taarifa zako binafsi kwa mtu yeyote, ikijumuisha kwa madhumuni ya matangazo.

Tuna uwazi kuhusu data tunayokusanya na sababu za kukusanya.

Tunayawekea lebo bayana matangazo na maudhui yaliyodhaminiwa katika mifumo yetu na kukurahisishia kuelewa ni kwa nini matangazo mahususi yanaonyeshwa, maelezo gani yanayotumika na jinsi unavyoweza kudhibiti hali yako ya utumiaji wa matangazo katika Google.

Kwa mfano, kwa kutumia huduma ya Tafuta, YouTube na Gundua, Kituo Changu cha Matangazo hukuonyesha maelezo yanayotumiwa kwenye matangazo na kufanya iwe rahisi kwako kudhibiti maelezo hayo ili matumizi yake yakufae.

Tunakurahisishia ili uweze kudhibiti taarifa yako binafsi.

Unadhibiti maelezo yako na jinsi yanavyotumika kwa madhumuni ya utangazaji. Shughuli yako kwenye Google — kama vile tovuti unazotembelea na vitu ulivyotafuta — hutumika ili kukupa hali bora zaidi ya utumiaji inayokufaa kwenye bidhaa zetu zote, ikiwa ni pamoja na matangazo, kulingana na mapendeleo yako.

Kituo Changu cha Matangazo hukuruhusu kuwekea mapendeleo hali yako ya utumiaji wa matangazo kwenye Huduma ya Tafuta na Google, Gundua na YouTube ili uone biashara na mada nyingi unazopenda na chache ya zile usizopenda. Unaweza pia kuchagua kupunguza matangazo kuhusu baadhi ya matangazo yaliyo na mada nyeti, ikiwa ni pamoja na pombe, kuchumbiana, kamari, ujauzito, malezi na upunguzaji wa uzito.

Unaweza kuzima mipangilio ya kuweka mapendeleo ya matangazo na ufute kabisa data ya shughuli inayohusiana na akaunti yako wakati wowote kwenye mipangilio ya data na faragha.

Tunapunguza kiwango cha data tunayochukua ili kulinda faragha yako zaidi.

Kamwe, hatutumii maelezo nyeti kama vile ya afya, mbari, dini au mwelekeo wa kingono ili kufanya matangazo yakufae zaidi.

Kamwe, hatutumii maudhui uliyotayarisha na kuhifadhi katika programu kama vile Hifadhi, Gmail na Picha kwa madhumuni yoyote ya matangazo. Na ili kulinda zaidi faragha yako, tulifanya kipengele cha kufuta kiotomatiki kuwa chaguomsingi kwa mipangilio yetu ya shughuli ya msingi. Hii inamaanisha kuwa data ya shughuli inayohusishwa na akaunti yako itafutwa kiotomatiki na kwa mfululizo baada ya miezi 18, badala ya kuhifadhiwa hadi utakapochagua kuifuta.

Kila wakati tunatafuta njia za kuwaweka watoto wawe salama zaidi wakiwa wanavinjari mtandaoni na haturuhusu kipengele cha kuweka mapendeleo ya matangazo kwa watoto ambapo tunajua kuwa wako chini ya umri wa miaka 18.

Tunakulinda kwa kubuni bidhaa zilizo salama kwa chaguomsingi.

Kulinda faragha na data yako ni jambo la msingi katika kazi ya Google. Ndiyo maana bidhaa zote za Google zinaendelea kulindwa na mojawapo ya miundombinu ya usalama ambayo ni thabiti zaidi ulimwenguni. Usalama huu uliojumuishwa husaidia kutambua na kuzuia hatari za mtandaoni, ikijumuisha ulaghai na majaribio ya kupata taarifa binafsi kupitia matangazo ya ulaghai, ili kusaidia kudumisha usalama wa maelezo yako.

Pia, ili kukusaidia uendelee kuwa salama, tunathibitisha watangazaji kote duniani na tunajitahidi kugundua watendaji wabaya na kudhibiti majaribio yao ya kujiwakilisha kwa njia ya uongo. Unaweza kupata maelezo zaidi kwa kutembelea kituo chetu cha utafutaji cha matangazo yote yanayoonyeshwa na watangazaji waliothibitishwa kwenye Kituo cha Uwazi kuhusu Watangazaji.

Tunaunda teknolojia bora za faragha na kuzishiriki na wengine.

Unapaswa kufurahia hali yako ya utumiaji mtandaoni bila kuwa na wasiwasi kuhusu ni taarifa gani za binafsi zinakusanywa na anayezikusanya. Ndio maana timu za Google zinashirikiana na sekta pana kutekeleza mpango wa Mazingira ya faragha unaolenga kufanya utaratibu wa sasa wa ufuatiliaji kuwa uliopitwa na wakati na kuzuia mbinu za ufuatiliaji kwa njia ya siri, kama vile ukusanyaji wa alama bainifu.

Chagua hali ya kuona matangazo
inayokufaa.

Njia mpya rahisi za kudhibiti matangazo unayoona.

Jaribio la ukurasa wa Kituo Changu cha Matangazo, wenye vidhibiti vya kuweka mapendeleo kwenye hali ya matangazo unayoona

Vidhibiti vya Matangazo Kwenye Google

Ukitumia Kituo changu cha Matangazo, ni rahisi zaidi kudhibiti matangazo unayoyaona kwenye huduma ya Tafuta na Google, YouTube na kipengele cha Gundua.

Kituo Changu cha Matangazo hukurahisishia mchakato wa kudhibiti taarifa zinazotumiwa kukuonyesha matangazo. Hii ni pamoja na taarifa zinazohusishwa na Akaunti yako ya Google na jinsi tunavyokadiria mambo yanayokuvutia kulingana na shughuli zako. Unaweza pia kutumia Kituo Changu cha Matangazo kuweka mapendeleo kwenye hali ya matangazo unayoyaona ili uone matangazo mengi zaidi kutoka chapa unazozipenda na upunguze yale ya chapa usizozipenda. Unaweza pia kufuta kabisa data ya shughuli inayohusiana na akaunti yako wakati wowote.

Vidhibiti vya Matangazo Nje ya Google

Tumia Mipangilio ya Matangazo kudhibiti matangazo yako kwenye tovuti na programu za wengine

Kama sehemu ya hali yako ya kuona matangazo mtandaoni, huenda ukaona matangazo kutoka kwa biashara zinazotumia Google kutangaza kwenye tovuti na programu fulani. Ili udhibiti matangazo haya, tembelea Mipangilio ya Matangazo ili udhibiti kwa urahisi taarifa zinazotumiwa kukuonyesha matangazo. Hii ni pamoja na taarifa ambazo umeweka kwenye Akaunti yako ya Google, jinsi tunavyokadiria mambo yanayokuvutia kulingana na shughuli zako na jinsi unavyotagusana na matangazo ya watangazaji wengine wanaotumia mfumo wetu wa utangazaji ili kuonyesha matangazo.

Zima matangazo yaliyowekewa mapendeleo wakati wowote unaotaka

Unaweza pia kuzima kabisa matangazo yaliyowekewa mapendeleo. Bado utaona matangazo, lakini huenda yasilingane sana na mambo yanayokuvutia. Mipangilio yako itatumika kwenye kifaa chochote ulichotumia kuingia katika Akaunti yako ya Google.

Pata maelezo zaidi kuhusu
matangazo
unayoonyeshwa.

Kwa nini unaonyeshwa tangazo hili

Angalia data tunayotumia kuonyesha matangazo

Kipengele cha “Kwa nini unaonyeshwa tangazo hili” kinakusaidia uelewe ni kwa nini unaonyeshwa tangazo husika. Kwa mfano, unaweza kugundua kuwa unaonyeshwa tangazo la kamera kwa sababu ulitafuta kamera, kutembelea tovuti za upigaji picha au kubofya matangazo ya kamera hapo awali.

Jaribio la ukurasa wa “Ni nani aliyelipia tangazo hili” ndani ya Kituo Changu cha Matangazo linaloonyesha kiasi cha pesa ambacho mtangazaji alilipia tangazo husika

Uthibitishaji wa utambulisho wa mtangazaji

Pata maelezo kuhusu watangazaji wanaokuonyesha matangazo

Ili kukupa maelezo zaidi kuhusu anayekuonyesha matangazo, tunajitahidi kuthibitisha utambulisho wa watangazaji kwenye mifumo yetu. Kama sehemu ya mpango huu, watangazaji wanahitajika kukamilisha mpango wa uthibitishaji ili waweze kununua matangazo kwenye Google na utaona fumbuzi za matangazo zinazoorodhesha jina na nchi ya mtangazaji.

Iwapo ungependa kupata maelezo zaidi – kama vile matangazo yapi yalionyeshwa katika eneo fulani au muundo wa tangazo – unaweza kutembelea Kituo cha Uwazi kuhusu Watangazaji, unachoweza kutafuta matangazo yote kwenye huduma za YouTube, Tafuta na Google na kipengele cha Gundua, yanayotoka kwa watangazaji waliothibitishwa. Unaweza kufikia Kituo cha Uwazi kuhusu Watangazaji moja kwa moja au kwa kutembelea Kituo changu cha matangazo kupitia menyu ya nukta tatu iliyo karibu na matangazo unayoyaona.

Tembelea Kituo cha Uwazi kuhusu Watangazaji

Pata maelezo zaidi kuhusu maswali ambayo watu wanauliza kuhusu matangazo.

Google hutumia data gani kwa ajili ya matangazo?

Tunatumia shughuli zako kwenye Google – kama vile tovuti unazotembelea, programu unazotumia na vitu ulivyotafuta – ili kukupa hali bora zaidi ya utumiaji inayokufaa kwenye bidhaa zetu zote, ikiwa ni pamoja na matangazo.

Hatutumii kamwe taarifa nyeti kama vile za afya, mbari, dini au mwelekeo wa kingono ili kufanya matangazo unayoona yakufae zaidi. Pia, hatutumii data kutoka katika Hifadhi, Gmail na Picha kwenye Google kwa ajili ya matangazo.

Unaweza kudhibiti taarifa zinazotumiwa kuweka mapendeleo kwenye matangazo na udhibiti mapendeleo yako ya matangazo kwa kutumia kipengele cha Kituo Changu cha Matangazo.

Kwa nini Google inatumia taarifa zangu kwa ajili ya utangazaji?

Google hutumia taarifa zako kukuonyesha matangazo ambayo tunafikiri kuwa yanahusiana na mambo yanayokuvutia kulingana na shughuli zako au kukusaidia kugundua kitu kipya.

Kwa mfano, ikiwa unatafiti kuhusu magari mapya, itafaa zaidi kuona matangazo yanayoangazia ofa kutoka kwa wauzaji wa eneo unakoishi badala ya kuona matangazo ya jumla kuhusu fanicha za roshani au vyakula vya wanyama vipenzi.

Unaweza kudhibiti data yako kila wakati ukitumia zana za faragha ambazo ni rahisi kutumia na ni chaguo lako kushiriki taarifa na Google na kuamua jinsi zinavyotumiwa kwa ajili ya utangazaji.

Je, Google husoma barua pepe zangu au kusikiliza mazungumzo yangu ya simu ili inionyeshe matangazo?

Hapana. Barua pepe na mazungumzo yako ni binafsi na ya faragha. Hatukuonyeshi matangazo kulingana na mambo unayoandika kwenye barua pepe zako, unachosema kwenye mazungumzo ya simu au unachohifadhi katika huduma kama vile Hifadhi ya Google.

Je, Google huuza taarifa zangu kwa watangazaji?

Hapana.

Hatuuzi kamwe taarifa zako binafsi kwa mtu yeyote.

Je, ninaweza kuzima kabisa kipengele cha matangazo yaliyowekewa mapendeleo?

Ndiyo. Unaweza kutembelea Kituo Changu cha Matangazo ili usasishe mapendeleo yako au uzime kipengele cha kuweka mapendeleo ya matangazo.

Ukichagua kutoona matangazo yaliyowekewa mapendeleo, bado utaendelea kuona matangazo, lakini yatakuwa hayakufai sana.

Gundua mbinu nyingi tunazotumia
kuimarisha usalama wako mtandaoni.