Kubuni hali za utumiaji
zinazofaa familia.

Tunabuni vipengele maalum – kama vile vichujio mahiri, vizuia tovuti na ukadiriaji wa maudhui – kwenye baadhi ya bidhaa zetu ili kuzifanya ziridhishe zaidi familia yako.

Hali ya utumiaji wa kompyuta kibao yenye
maudhui ya kusaidia watoto
kugundua, kubuni na kukua.*
Skrini inayoangazia Google Kids Space iliyo na mhusika wa katuni ya mtoto na programu iliyoratibiwa inayoangaziwa na kiumbe anayeruka.
Bidhaa unazopenda,
zilizobuniwa kwa ajili ya familia.
Skrini inayoangazia video tofauti za watoto kuchagua kwenye YouTube Kids

YouTube Kids

Gundua ulimwengu wa mafunzo na burudani ukitumia YouTube Kids

Tumebuni YouTube Kids iwe huduma salama kwa ajili ya watoto ili wagundue mambo yanayowavutia kupitia video za mtandaoni. Unaweza kupata video zinazofaa familia zinazoangazia mada zote tofauti kwenye vifaa vyako vyote, iwe umepakua programu ya YouTube Kids, kututembelea kwenye wavuti au kutazama YouTube Kids katika televisheni yako inayoweza kuunganisha kwenye intaneti.

Simu inayoangazia kichupo cha watoto kwenye Google Play iliyo na maudhui yaliyoidhinishwa na mwalimu

Google Play

Maudhui “yaliyoidhinishwa na walimu” kwa ajili ya mtoto wako kwenye Google Play

Tunashirikiana na wataalamu wa elimu na walimu kote nchini, ili kukusaidia kupata maudhui ambayo ni sahihi kwa watoto wako. Vinjari kichupo chetu cha Watoto kwenye Duka la Google Play ili upate programu “zilizoidhinishwa na Walimu” ambazo hufunza na kuburudisha. Kwenye ukurasa wa programu wa maelezo, unaweza kuona kwa nini walimu huzipa programu ukadiriaji wa kiwango cha juu na uangalie ukadiriaji wa maudhui ili uelewe iwapo programu inafaa kwa umri wa watoto. Unaweza pia kuona kama programu ina matangazo, inaruhusu ununuzi wa ndani ya programu au inahitaji ruhusa za kifaa.

Tunawasimamia wasanidi programu wanaobuni programu za watoto katika kiasi kikubwa kwa kutumia sera zetu za wasanidi programu za Duka la Google Play.

Google Home iliyo na viputo vya maneno: Mtu anasema, "Ok Google, nisimulie hadithi." Programu ya Mratibu wa Google inajibu "Hakika, hii ni hadithi kuhusu "Mbweha na Kunguru" kutoka Storynory kwenye Vitabu vya Google Play..."

Mratibu wa Google

Furaha kwa familia yote kwa usaidizi kutoka kwenye programu ya Mratibu wa Google

Programu yako ya Mratibu hurahisisha hatua ya kupata burudani ya familia yote ili mfurahie pamoja. Gundua michezo na shughuli zinazofaa familia, iliyobuniwa kupitia mpango wetu wa Vitendo Vinavyolenga Familia au sikiliza hadithi unazopenda kabla ya kulala kwa kuiambia tu programu ya Mratibu wako ikusimulie hadithi. Sikiza muziki ambao familia nzima inaweza kufurahia baada ya kuweka Vichujio na utumie Wakati wa kupumzika kwenye kifaa chako ili kusitisha na kunufaika na muda wenyu pamoja.

Wataalamu wamekagua shughuli zetu zote za Vitendo Vinavyolenga Familia ili kubaini ufaafu kwa familia, lakini hakuna mfumo usio na kasoro. Maudhui yasiyofaa yanaweza kupatikana, kwa hivyo tunajitahidi kuboresha kinga zetu.

Kuwapa wanafunzi na waelimishaji zana za mafunzo ambayo ni salama mtandaoni.
Kompyuta ya kupakata inayoangazia bidhaa za Google ambazo ni sehemu ya Google Workspace

Google Workspace

Kubuni mazingira salama zaidi ya mafunzo kwenye madarasa

Google Workspace for Education huwasaidia walimu na wanafunzi wawasiliane kwa njia salama kwenye vifaa vyote. Huduma zake za msingi hazijumuishi matangazo na hatutumii taarifa zozote binafsi za watumiaji katika shule za msingi na za upili (K–12) kuwaonyesha matangazo. Pia, tunatoa zana za kuwasaidia wasimamizi waweke sera kuhusu shughuli zinazofaa na kusaidia kuwalinda wanafunzi wanaotumia Akaunti za Google shuleni. Tumejitolea kuzipa shule zana na nyenzo zinazohitaji ili kufanya uamuzi wa busara kuhusu huduma za Google Workspace for Education zinazotumiwa na wanafunzi.

Chromebook mbili, moja nyuma ya nyingine.

Chromebook

Kufanya darasa liwe salama

Mamilioni ya wanafunzi wanatumia Chromebook – kompyuta za kupakata za Google – madarasani. Wasimamizi wanaweza kudhibiti mipangilio ya makundi ili kuwapa wanafunzi utendaji au uwezo wanaohitaji. Vipengele vyetu vya faragha na usalama husaidia kulinda taarifa binafsi ya watoto na vimesaidia kufanya Chromebook iwe chaguo bora Marekani katika shule za K–12 na shule nyingi katika nchi zingine.

Vidhibiti vya Wazazi

Pata maelezo kuhusu jinsi Google husaidia familia kuweka sheria dijitali za msingi na kuweka desturi bora mtandaoni.