Kulinda faragha yako
huanza na miundombinu ya usalama
ambayo ni thabiti zaidi ulimwenguni.

Bidhaa zote za Google zinalindwa kila wakati na mojawapo ya miundombinu ya usalama ambayo ni thabiti zaidi ulimwenguni. Usalama huu uliojumuishwa hutambua na kuzuia kiotomatiki hatari za mtandaoni, ili upate uhakika kuwa taarifa yako ya faragha iko salama.

Tunakulinda mtandaoni
kupitia usalama
unaosasishwa kila mara.

Usimbaji fiche

Usimbaji fiche hudumisha faragha na usalama wa data inapotumwa

Usimbaji fiche huboresha kiwango cha usalama na faragha kwenye huduma zetu. Unapotuma barua pepe, kushiriki video, kutembelea tovuti au kuhifadhi picha zako, data unayotengeneza hupitia kwenye kifaa chako, huduma za Google na vituo vyetu vya data. Tunalinda data hii kwa kutumia vidhibiti vingi vya usalama, ikiwa ni pamoja na teknolojia maarufu ya usimbaji fiche kama vile HTTPS na TLS.

Arifa za Usalama

Arifa hima za usalama husaidia kulinda maelezo yako ya faragha

Tutakuarifu kwa hima tukitambua kitu ambacho tunaona kuwa unapaswa kujua kuhusu, kama vile hatua ya kutiliwa shaka ya kuingia katika akaunti au tovuti, faili au programu hasidi na tutakupa mwongozo wa kukusaidia kuimarisha usalama wako. Kwa mfano, kwenye Gmail, tutakuonya kabla ya kupakua kiambatisho ambacho kinaweza kuhatarisha usalama wako au iwapo mtu ataingia katika akaunti yako akitumia kifaa ambacho hakihusishwi nawe. Tukitambua shughuli zinazotiliwa shaka katika akaunti yako, tutatuma arifa kwenye kikasha chako au kwenye simu yako ili uweze kulinda akaunti yako haraka zaidi.

Kuzuia matangazo mabaya

Kuzuia matangazo hasidi na yanayopotosha kabla yakufikie

Usalama na hali yako ya utumiaji mtandaoni inaweza kuathiriwa na matangazo yaliyo na programu hasidi, yanayofunika maudhui unayojaribu kuona, yanayotangaza bidhaa bandia, au kukiuka vinginevyo sera zetu za matangazo. Tunachunguza tatizo hili kwa makini. Kila mwaka, tunazuia mamilioni ya matangazo yasiyofaa – kwa wastani takribani matangazo 100 kwa kila sekunde – kupitia usaidizi wa wakaguzi wa moja kwa moja na programu za hali ya juu. Tunakupa pia zana za kuripoti matangazo yanayokera na kudhibiti aina za matangazo unayoona. Na tunachapisha kila wakati maarifa na mbinu bora zaidi za kuimarisha usalama wa intaneti kwa manufaa ya kila mtumiaji.

Mnara wa seva za data ulio na nembo ya Wingu la Google katika sehemu ya juu

Usalama wa Wingu

Miundombinu yetu ya wingu hulinda data wakati wote

Kuanzia vituo maalum vya data hadi kebo zetu baharini ambazo husafirisha data kati ya mabara, Google hutumia mojawapo ya miundombinu ya wingu ambayo ni thabiti na salama zaidi ulimwenguni. Hufuatiliwa kila wakati ili kulinda data yako na kuifanya ipatikane. Na kukitokea tukio la kukatiza, huduma za mfumo zinaweza kuhamishwa kiotomatiki na papo hapo kutoka eneo moja hadi lingine ili ziweze kuendelea bila kukatizwa.

ZANA ZA UTHIBITISHAJI

Kuingia kwa njia salama katika akaunti zako zote za mtandaoni

Akaunti za mtandaoni hutoa huduma muhimu maalum, lakini hatua ya kuingia katika akaunti hizo ina hatari kubwa zaidi za usalama siku hizi. Kila siku, manenosiri mengi zaidi hufichuliwa katika matukio ya ufichuzi haramu wa data, hali ambayo inaweza kuhatarisha taarifa yako binafsi.

Huduma na zana zetu za uthibitishaji zilizojumuishwa zimebuniwa ili kukusaidia uingie katika huduma na programu uzipendazo kwa haraka na kwa njia salama.

Tunalinda bidhaa
unazotumia kila siku.
Gundua mbinu nyingi za
kuimarisha usalama wako mtandaoni.