Njia salama zaidi ya kuingia katika akaunti zako zote za mtandaoni.

Mchakato wa kuingia katika akaunti zako zote za mtandaoni haupaswi kuwa mgumu. Unapaswa kuwa wa haraka na rahisi bila kukutia wasiwasi kwamba taarifa binafsi za akaunti yako zinaweza kuwa hatarini.

Zana zetu za uthibitishaji zilizojumuishwa zimebuniwa ili kukusaidia uingie katika akaunti kwenye huduma na programu uzipendazo kwa haraka na kwa njia salama.

Kukagua Manenosiri: Imarisha usalama wa Akaunti yako ya Google

Linda akaunti zako zote za mtandaoni kwa kufanya Ukaguzi wa Manenosiri. Pima uthabiti wa manenosiri yako, angalia iwapo umetumia nenosiri lolote zaidi ya mara moja na ufahamu iwapo kuna manenosiri yaliyoathiriwa.

Fanya Ukaguzi
Gundua mbinu za ziada tunazotumia
kuimarisha usalama wako mtandaoni.