Tunakusaidia udhibiti maudhui
yanayofaa familia yako mtandaoni.

Watoto wa siku hizi wanakua na teknolojia. Watoto wa zamani walikuwa nyuma ya teknolojia. Kwa hivyo, tunashirikiana moja kwa moja na wataalamu na waelimishaji ili kukusaidia udhibiti na utumie teknolojia kwa namna inayofaa familia yako.

Help keep your family safer online.
Picha inayoonyesha simu ya mtoto anayeitwa Benjamin ikiwa imefungwa hadi saa moja asubuhi kwa kutumia Vidhibiti vya Wazazi. Kipimo cha matumizi ya kila siku kimeonyeshwa chini yake.

FAMILY LINK

Weka mipangilio ya udhibiti wa wazazi

Family Link hukusaidia udhibiti vifaa na akaunti ya mtoto wako anapovinjari mtandaoni. Weka vikomo vya muda wa kutumia kifaa, dhibiti maudhui ambayo mtoto wako anaweza kuona na ufahamu mahali alipo akiwa na kifaa chake.

Kudumisha hali
ya utumiaji inayofaa familia
kwenye
bidhaa zetu zote.
Skrini inayoonyesha Google Kids Space iliyo na mhusika wa katuni ya mtoto na programu iliyoratibiwa inayoangaziwa na kiumbe anayeruka.

Hali za Utumiaji Zinazofaa Familia

Gundua vipengele vilivyobuniwa kwa ajili ya familia

Tunabuni vipengele maalum – kama vile vichujio mahiri, vizuia tovuti na ukadiriaji wa maudhui – kwenye bidhaa zetu nyingi katika Duka la Google Play, programu ya Mratibu, YouTube na zaidi ili kuzifanya zifurahishe familia zaidi.

Dhibiti maudhui yanayofaa
familia yako mtandaoni.