Faragha yako inalindwa na
kanuni za data zenye uwajibikaji.

Data huwa muhimu katika kuboresha bidhaa na huduma unazotumia kila siku. Tumejitolea kushughulikia data kwa kuwajibika na kulinda faragha yako kwa kutumia itifaki thabiti na teknolojia bunifu za faragha.

KUPUNGUZA DATA

Kupunguza taarifa binafsi zinazotumiwa na kuhifadhiwa

Tunaamini bidhaa zinapaswa kuhifadhi tu maelezo yako kwa muda ambao yanakufaa – iwe ni kuweza kupata maeneo unayopenda kwenye Ramani au kupata mapendekezo ya mambo ya kutazama kwenye YouTube.

Mara ya kwanza unapowasha Kumbukumbu ya Maeneo Yangu – ambayo imezimwa kwa chaguomsingi – chaguo lako la kufuta kiotomatiki litawekwa kuwa miezi 18 kwa chaguomsingi. Kufuta kiotomatiki Historia ya Shughuli kwenye Wavuti na Programu kutakuwa pia miezi 18 kwa chaguomsingi katika akaunti mpya. Hii inamaanisha kuwa data ya shughuli zako itafutwa kiotomatiki na kila mara baada ya miezi 18, badala ya kuhifadhiwa hadi utakapochagua kuifuta. Unaweza kuzima mipangilio hii au kubadilisha mipangilio ya kufuta kiotomatiki wakati wowote.

KUZUIA UFIKIAJI

Hatuuzi taarifa zako binafsi kamwe na tunakupa uwezo wa kudhibiti anayeweza kuzifikia

Tumejitolea kulinda data yako dhidi ya wahusika wengine. Ndiyo maana sera yetu thabiti hairuhusu uuzaji wa taarifa binafsi kwa mtu yeyote. Hatushiriki taarifa zinazokutambulisha binafsi kwa watangazaji, kwa mfano jina au anwani yako ya barua pepe isipokuwa utuombe kufanya hivyo. Kwa mfano, ukiona tangazo la duka la maua lililo karibu nawe kisha uchague “gusa ili upige simu”, tutaunganisha simu yako na tunaweza kushiriki nambari yako ya simu na duka hilo la maua. Iwapo unatumia kifaa cha Android, tunahitaji programu za wengine ziombe ruhusa yako ili zifikie aina fulani za data – kama vile picha, anwani au eneo uliko.

UVUMBUZI WA FARAGHA

Teknolojia kuu za faragha husaidia kuhifadhi taarifa yako binafsi kwa faragha

Tunaendelea kuvumbua teknolojia mpya zinazolinda taarifa yako ya faragha bila kuathiri hali yako ya utumiaji wa bidhaa zetu.

Mafunzo shirikishi ni teknolojia ya kupunguza data, iliyobuniwa katika Google, inayotoa mafunzo ya miundo ya mashine inayosaidia vipengele vingi vyetu muhimu, kama vile utabiri wa maneno, kwenye kifaa chako. Mbinu hii mpya husaidia kuhifadhi faragha yako kwa kuweka hali inayowafaa watumiaji kwenye bidhaa zetu huku tukihifadhi taarifa binafsi kwenye vifaa vyako.

Tunatumia mbinu za kuficha utambulisho wa data ili kulinda data yako huku tukiboresha huduma zetu kwa ajili yako. Kwa mfano, tunajumlisha na kuficha utambulisho wa data kutoka mamilioni ya watumiaji ili kupendekeza njia mbadala zinazoweza kukufikisha nyumbani haraka.

Ili kutoa vipengele kama vile shughuli kwenye Ramani, tunatumia teknolojia ya kuficha utambulisho wa data, inayoitwa faragha kwa kuchanganya data, inayoweka misimbo kwenye taarifa yako ili isiweze kutumiwa kukutambulisha.

Ukaguzi wa faragha

Itifaki thabiti za faragha hufuatwa
kwenye hatua zote za kubuni bidhaa

Faragha ni muhimu katika jinsi tunavyobuni bidhaa zetu, kwa kutumia viwango thabiti vya faragha kuongoza katika kila hatua ya kubuni. Kila bidhaa na kipengele kinatii viwango hivi vya faragha, ambavyo hutekelezwa kupitia ukaguzi wa faragha kwa kina. Pata maelezo zaidi katika Sera yetu ya Faragha.

UWAZI WA DATA

Kurahisisha mchakato wa kuona na kufuta data yako

Ni wewe unayemua jinsi utakavyotumia bidhaa na huduma zetu. Ili kukusaidia kufanya uamuzi bora kuhusu data tunayohifadhi, kushiriki au kufuta, tunarahisisha kuelewa data inayokusanywa na sababu za kuikusanya.

Kwa mfano, kwa kutumia Dashibodi, unaweza kuona muhtasari wa bidhaa za Google unazotumia na mambo unayohifadhi kama vile barua pepe na picha zako. Na kwa kutumia 'Shughuli Zangu', ni rahisi kuona na kufuta data inayokusanywa kutoka shughuli zako kwenye huduma za Google, ikiwemo mambo ambayo umetafuta, kuona na kutazama.

UWEZO WA KUBEBA DATA

Kukuwezesha uchukue data yako

Kila mtumiaji anapaswa kuwa na uwezo wa kufikia maudhui ambayo ameshiriki nasi – wakati wowote na kwa sababu yoyote. Ndiyo maana tulibuni 'Pakua Data Yako' – ili uweze kupakua picha, barua pepe, anwani na alamisho zako. Ni chaguo lako kutoa nakala ya data yako, kuhifadhi nakala au kuihamishia kwenye huduma nyingine.

Una udhibiti wa data inayohifadhiwa kwenye Akaunti yako ya Google kila wakati. Pata maelezo zaidi hapa.

Tumejitolea kutii
sheria zinazotumika za ulinzi wa data

Tunajitahidi kila wakati kutii kanuni husika za faragha. Kwa miaka mingi, tumefanya kazi kwa karibu na mamlaka za ulinzi wa data kote duniani na tumetekeleza ulinzi thabiti wa faragha unaolingana na mwongozo wao. Na tunaendelea kujitahidi kusasisha mifumo na sera zetu kadri sheria za faragha zinavyotekelezwa kote duniani.

Pata maelezo zaidi
Gundua mbinu nyingi tunazotumia
kuimarisha usalama wako mtandaoni.