Kanuni zetu za faragha

Kubuni bidhaa zinazozingatia faragha kwa kila mtu.

Tunabuni bidhaa ambazo zinazingatia faragha na zinamfaa kila mtu. Hii inamaanisha tunazingatia kwa umakini data tunayotumia, jinsi tunavyoitumia na tunavyoilinda.

Kanuni hizi huongoza jinsi tunavyobuni bidhaa zetu, michakato yetu na watu wetu ili kuhakikisha usalama na faragha ya data na kukupa udhibiti wa taarifa zako.

1.

Kamwe Hatuuzi taarifa zako binafsi kwa yeyote.

Tunatumia data ili kufanya bidhaa za Google zikufae katika matukio muhimu. Kama vile kukusaidia kupata mgahawa ulio karibu au njia ya kwenda nyumbani inayookoa mafuta.

Pia, tunatumia data kuonyesha matangazo yanayofaa zaidi. Ingawa matangazo haya yanatuwezesha kukupatia bidhaa bila gharama kwa kila mtu, ni muhimu kubainisha kwamba kamwe hatuuzi taarifa binafsi kwa mtu yeyote, ikiwa ni pamoja na kwa madhumuni ya matangazo. Haturuhusu kabisa.

2.

Tunazingatia uwazi kuhusu data tunayokusanya na sababu za kukusanya.

Tunataka ujue kuhusu data tunayokusanya, jinsi tunavyoitumia na sababu za kuikusanya. Uwazi ni muhimu, kwa hivyo tunafanya iwe rahisi kupata na kuelewa maelezo haya. Kwa njia hii, unaweza kufanya maamuzi bora kuhusu jinsi unavyotumia bidhaa za Google.

3.

Tunafanya iwe rahisi kwako kudhibiti taarifa zako binafsi.

Hii inamaanisha kuwa unaweza kuchagua kwa urahisi mipangilio ya faragha inayokufaa na unaweza kudhibiti taarifa binafsi ambazo umeshiriki na Google wakati wowote unapotaka, ikiwa ni pamoja na kukagua data yako, kuipakua na kuihamishia kwenye huduma nyingine ukipenda au ufute kabisa.

4.

Tunapunguza kiwango cha data tunayotumia ili kulinda faragha yako zaidi.

Kamwe hatutumii maudhui unayotunga na kuhifadhi kwenye programu kama vile Hifadhi, Gmail na Picha kwa madhumuni ya kutangaza na kamwe hatutumii taarifa nyeti kama vile za afya, mbari, dini au mwelekeo wa kingono ili kufanya matangazo yakufae zaidi.

Pia, tumefanya vidhibiti vya kipengele cha kufuta kiotomatiki kuwa chaguomsingi unapojisajili kwenye akaunti ya Google, ili mara kwa mara tuweze kufuta data ya shughuli zako za mtandaoni inayohusishwa na akaunti yako ya Google, kama vile mambo ambayo umetafuta na kutazama.

5.

Tunakulinda kwa kubuni bidhaa zilizo salama kwa chaguomsingi.

Unapotumia bidhaa zetu, unatuamini kutupatia maelezo yako na ni wajibu wetu kuheshimu uaminifu wako. Ndiyo maana tunatumia mojawapo ya mifumo thabiti zaidi ya usalama duniani ili kulinda data yako.

Tumebuni bidhaa zetu kuwa salama kwa chaguomsingi na kila mara tunaimarisha mbinu zetu za usalama ili kutambua na kuzuia vitisho vya mtandaoni vinavyobadilika badilika, kama vile watendaji wabaya wanaojaribu kuiba taarifa zako binafsi, kabla wakufikie.

6.

Tunaunda teknolojia bora za faragha na kuzishiriki na wengine.

Kufanya intaneti iwe wazi, ya faragha na salama ni jambo la msingi tunalofanya. Usalama wako wa mtandaoni haupaswi kuwa tu kwenye Google - unapaswa kuwa kwenye intaneti yote. Ndiyo maana tunaendelea kuvumbua teknolojia za faragha na kuzifanya zipatikane kwa watu wengi. Tunashiriki maarifa, ujuzi na zana zetu na washirika, mashirika na washindani, kwa sababu kuimarisha usalama wa mtandao kunahitaji ushiriki wa kila mtu.

Gundua jinsi Google inavyosaidia
kulinda usalama wa kila mtu mtandaoni.