Kutengeneza teknolojia imfae kila mtu kunamaanisha kulinda kila mtu anayeitumia.

Google ilianzishwa kwa imani kwamba kila kitu tunachofanya kinapaswa kiheshimu mtumiaji kila wakati. Kadri intaneti inavyoendelea ndivyo tunapaswa kuimarisha teknolojia zetu za usalama na zana za faragha ili kusaidia kudumisha usalama wako na wa familia yako mtandaoni.

Gundua mambo tunayofanya ili kuimarisha usalama wako

Usalama Wako

Tunakulinda mtandaoni kwa kutumia zana bora zaidi za usalama.

Kila kitu tunachounda kimelindwa kwa teknolojia thabiti za usalama zinazojumuishwa ndani ya mfumo. Teknolojia hizi zinakusaidia utambue na uzuie vitisho kama vile taka, programu hasidi na virusi ili visikufikie. Na tunashiriki teknolojia hizi za usalama na washirika na washindani wetu. Hali hii inaboresha viwango vya sekta vinavyosaidia kuimarisha usalama wa kila mtu mtandaoni.

Pata maelezo zaidi

Faragha Yako

Tunaunda faragha inayomfaa kila mtu.

Data hufanya huduma za Google ziwafae zaidi watumiaji. Hata hivyo, ni wewe unaamua jinsi ungependa tutumie maelezo hayo. Tunakujulisha kuhusu data tunayokusanya, jinsi tunavyoitumia na sababu za kuitumia. Na tunaunda vidhibiti thabiti vya data kwenye Akaunti yako ya Google. Hali hii inakuruhusu uchague mipangilio ya faragha ambayo inakufaa.

Pata maelezo zaidi

Kwa Ajili ya Familia

Tunakusaidia udhibiti maudhui yanayofaa familia yako mtandaoni.

Watoto wa siku hizi wanaendana na teknolojia. Watoto wa zamani walikuwa nyuma ya teknolojia. Kwa hivyo, tunafanya kazi moja kwa moja na wataalamu na waelimishaji ili kukusaidia kudhibiti na kutumia teknolojia kwa namna inayofaa familia yako.

Pata maelezo zaidi