Usalama
wa kuaminika.

Nufaika zaidi kutokana na hali yako ya kuvinjari, huku vipengele vya usalama vya Chrome vikikulinda dhidi ya programu hasidi na tovuti hatari.

Usalama uliojumuishwa

Ni salama kwa chaguomsingi

Ni salama kwa chaguomsingi

Chrome ni salama kwa chaguomsingi na inakulinda dhidi ya tovuti hatari na laghai ambazo zinaweza kuiba manenosiri yako au kuathiri kompyuta yako. Teknolojia za kina, kama vile utengaji wa tovuti, utaratibu wa kuwekea vikwazo na ulinzi dhidi ya wizi wa data binafsi unaotabirika, hulinda usalama wako na wa data yako.

Manenosiri thabiti na mahususi unapovinjari mtandaoni

Manenosiri thabiti na mahususi unapovinjari mtandaoni

Sahau manenosiri dhaifu na yanayojirudia ambayo yanaweza kufanya data yako ifichuke kwenye tovuti nyingi. Chrome inaweza kutengeneza manenosiri thabiti na mahususi na kuyajaza kiotomatiki kwa ajili yako unapovinjari mtandaoni kwenye simu ya mkononi au kompyuta yako ya kupakata. Chrome inaweza kukuonya ikiwa kitambulisho chako kimeathiriwa.

Daima imesasishwa

Chrome husasishwa kiotomatiki kila baada ya wiki sita, kwa hivyo utapata kila wakati marekebisho na vipengele vipya zaidi vya usalama. Kwa hitilafu muhimu za usalama, tutatuma arifa ya marekebisho ndani ya saa 24 – huhitaji kuchukua hatua yoyote.

Vidhibiti vya faragha

Hali fiche

Hali fiche

Hali fiche huondoa wasiwasi unaposhiriki kifaa chako na familia na marafiki zako. Vinjari katika Hali fiche na historia yako ya kuvinjari kwenye madirisha fiche hufutwa kwenye Chrome pindi unapoyafunga.

Angalizo la usalama

Angalizo la usalama la Chrome linaweza kuthibitisha faragha na usalama wa jumla wa hali yako ya kuvinjari. Hukufahamisha ikiwa manenosiri yoyote yaliyohifadhiwa kwenye Chrome yameathiriwa, kuripoti viendelezi hatari na kukusaidia kuhakikisha kuwa ulinzi wa usalama wako umesasishwa.

Vidhibiti vya faragha

Kuanzia kwa mipasho iliyowekewa mapendeleo, udhibiti rahisi wa manenosiri hadi matokeo ya utafutaji yanayofaa, hali yako ya utumiaji wa Chrome inaweza kufanywa ikufae zaidi. Weka mapendeleo ya hali yako ya utumiaji kwa kutumia vidhibiti vya usawazishaji na faragha vya Chrome, ikiwa ni pamoja na kudhibiti ruhusa za tovuti, kama vile ufikiaji wa kamera au mahali uliko.

Duka la Chrome
Pata maelezo zaidi
kuhusu Chrome.
Pata maelezo kuhusu jinsi usalama unavyojumuishwa kwenye
kila bidhaa tunayobuni.