Kuhakikisha
Intaneti salama na inayoaminika zaidi.
Leo, tuna timu za Google zinazoshughulikia faragha, usalama, uwajibikaji wa maudhui na usalama wa familia kote duniani. Vituo vyetu vya Uhandisi wa Usalama kwenye Google vilivyo Munich na Dublin, vinasaidia katika kuelekeza kazi hii ya usalama Mtandaoni, vikiongozwa na timu za wahandisi, wataalamu wa sera na wataalamu wa maudhui wenye uzoefu.
Kituo chetu cha Munich kinashughulikia kimahususi uhandisi wa usalama na faragha.
Kituo chetu cha Dublin kinashughulikia kimahususi uwajibikaji wa maudhui.
uhandisi wa usalama.
Tunazungumza na watu kote duniani ili tufahamu hofu yao kuhusu usalama kwenye Intaneti. Tunazipa timu zetu za wataalamu fursa, uhamasisho na usaidizi ili kubuni masuluhisho mapya ya kusaidia kuboresha usalama mtandaoni.
Tunauliza maswali na kusikiliza maoni ili tuelewe matukio ya sasa na ya baadaye yanayotishia usalama kwenye Intaneti
Tunasanidi masuluhisho mapya na yanayofaa ya uhandisi ili kukabili matatizo haya
Tunawezesha watu kujilinda kupitia zana, nyenzo na mikakati
Tunashirikiana na watunzi wa sera ili kushiriki maarifa na kukabili matatizo changamano