Kuelewa jinsi watu wanavyopokea unachounda.

Watafiti wa hali ya utumiaji hutafiti jinsi watu wanavyotumia bidhaa. Arne de Booij ni mtaalamu wa hali ya utumiaji na faragha mtandaoni. Stephan Micklitz ni Mkurugenzi wa Uhandisi wa Faragha na Usalama na anaangazia kuunda zana za faragha na usalama.

Arne de Booij, kama mtafiti wa hali ya utumiaji katika Google, unachanganua jinsi watumiaji wanavyotumia zana za faragha na usalama. Umejifunza nini?

Arne de Booij, Msimamizi wa Utafiti wa Hali ya Utumiaji wa Google: Inaweza kuonekana kuwa kawaida, lakini watu wanataka kuhisi wako salama mtandaoni. Wanataka data yao iwekwe kwa faragha. Katika miaka ya hivi karibuni, kadri intaneti inavyoongezeka kwa ukubwa na uchangamano, watu wametaka kujua kama wapo salama kwa kiasi gani na iwapo faragha yao imelindwa vyema. Hayo ni maswali ya maana kuuliza, ukizingatia jinsi tunavyotumia intaneti siku hizi na hadithi tunazosoma kuhusu kuvuja kwa data na kadhalika.

Katika mazungumzo: Arne de Booij (kushoto), Mtafiti wa Hali ya Utumiaji na Stephan Micklitz, mhandisi wa programu

Watu huwa na nyendo zipi mtandaoni kuhusiana na masuala ya faragha na usalama?

De Booij: Katika miaka michache iliyopita tumefanya utafiti uliowashirikisha watu walio katika nchi mbalimbali kote duniani na tumesikia kutoka kwao kwamba faragha ni muhimu sana. Kihistoria ukweli ni kwamba watu hawatumii muda mwingi kusoma taarifa ya faragha au kurekebisha mipangilio yao ya faragha. Utafiti mwingine unaonyesha kwamba watu hawasiti kuweka maelezo yao ya mawasiliano katika tovuti wasiyotambua – ili washiriki katika mashindano, kwa mfano. Kwa hivyo ni jukumu la makampuni kama vile Google kuhakikisha kuwa tumeelewa kabisa jinsi tunavyotumia data na kwamba tunawapa vidhibiti rahisi kutumia kudhibiti hali yao ya utumiaji mtandaoni kwa njia zinazowafaa.

"Ni jukumu letu kuwaelezea watu kwa njia ambayo wataelewa."

Arne de Booij

Stephan Micklitz kama mtu anayehakikisha faragha na usalama wa data, unapata hitimisho lipi kutokana na hili?

Micklitz: Tunalenga kuendelea kuunda huduma zinazowapa watumiaji udhibiti wa data yao wenyewe. Usalama na faragha ya data huonekana kuwa mada ambazo watu hawashughulikii sana hadi tatizo linapotokea – kwa mfano, akaunti yao inapodakuliwa au wanaposoma kwenye taarifa kuhusu jambo baya ambalo limefanyika. Jambo mujimu kwenye matukio hayo ni kwamba, watu wanajua jinsi ya kuangalia shughuli zao mtandaoni na wabadilishe manenosiri wakihitaji.

De Booij: Ukweli ni kwamba hakuna anayeamka asubuhi na kufikiria mwenyewe, “Ni vyema niangalie mipangilio yangu ya faragha kwenye Google Account sasa hivi.” Hali si hiyo. Usalama na faragha ya data ni mojawapo ya mambo ambayo wengi wetu hupuuza hadi baadaye. Ndiyo maana, katika miaka ya hivi karibuni, tumeanza kuwadokezea watu waangalie mipangilio yao mara kwa mara.

Kwa hivyo, unapata vipi maarifa yanayokusaidia kuunda bidhaa bora?

De Booij: Kuna mkusanyiko mzima wa chaguo. Tafiti za mtandaoni ni nzuri kwa kuchunguza jinsi watu wanavyotumia programu kama vile Akaunti ya Google. Iwapo unatafuta maoni na hisia, mahojiano ya mtu binafsi yanafaa zaidi. Ili kupata maelezo zaidi kuhusu tofauti za utamaduni, tunafanya utafiti kote duniani – kwenye barabara, katika studio za utafiti wa soko au hata nyumbani mwa watumiaji. Chaguo la mwisho ni la kuvutia hasa, kwa sababu hapo watu wanaweza kufikia vifaa na data yao wenyewe, hali ambayo inafanya tabia yao ya utumiaji inaaminika zaidi.

Arne de Booij (kushoto) alipata shahada katika saikolojia ya majaribio katika Chuo Kikuu cha Groningen na uzamivu wa kitaalamu katika uhandisi katika Chuo Kikuu cha Teknolojia cha Eindhoven. Anasema: “Watafiti wa Hali ya Utumiaji huhakikisha kuwa mahitaji ya watumiaji yanatambuliwa.”

Je, unaweza kutupatia mfano?

De Booij: Wakati mmoja, wafanyakazi wenzangu walitembelea mwanamke nyumbani kwake Japani kumwongelesha kuhusu Akaunti ya Google. Hakuwa anaifahamu huduma hii na alipoifungua, moja kwa moja aligeuza skrini kutoka upande tuliokuwa. Lakini alishangazwa sana kujifunza jinsi Akaunti ya Google inavyofanya kazi, jinsi angeweza kufuta taarifa na kuchagua jinsi Google inavyotumia data.

Stephan Micklitz, na wewe pia umewahi kuwa na mahojiano kama hayo?

Micklitz: Ndiyo! Kwa mfano, tulipokuwa tunatoa sampuli ya sasa ambayo ni Akaunti ya Google, tulitaka kuijaribu na kusikia maoni ya watu. Mshiriki wa kwanza alifungua ukurasa na kuuangalia kwa muda mrefu, bila kufanya chochote. Kisha mtu wa pili aliingia na akafanya hivyo hivyo. Nikafikiria, “Kumbe, mambo si kama nilivyonuia.” Ilikuwa wazi kuwa watumiaji hao hawakuelewa Dashibodi ya Google.

"Utafiti wa UX huchangia pakubwa katika harakati za utengenezaji."

Stephan Micklitz

Je, ulishughulikia tena kiolesura kwa sababu hiyo?

Micklitz: Mara kadhaa! Tuliendelea kushughulika hadi bidhaa ikaweza kufikiwa kwa haraka na kueleweka na watu hatimaye.

Basi utafiti wa UX research umekusaidia kuboresha huduma hizo?

Micklitz: Huchangia pakubwa katika harakati za utengenezaji. Hiyo ndiyo ilikuwa hali, kwa mfano, tunaposhughulikia Kidhibiti cha Akaunti Isiyotumika, ambayo sasa ni sehemu ya Akaunti ya Google. Inawaruhusu watumiaji kuamua kitakachofanyika kwenye data yao kama hajakuwa akifanya chochote kwa kipindi cha muda fulani. Bidhaa hii ilikuwa mpya kabisa; hakuna washindani wetu ambao walikuwa wameanzisha kitu kama hiki. Kwa hivyo tuliunda mfano, tukaujaribu na tukaunda mfano wa pili. Tulipitia mizunguko kadhaa ya mchakato huo kabla ya kuwa na bidhaa ambayo imepokelewa vizuri na watumiaji wetu.

Ni jambo la kuridhisha sana utafiti wako unapoleta mabadiliko makuu.

De Booij: Hilo ndilo jambo nzuri zaidi kuhusu kazi hii. Tunahakikisha kuwa mahitaji ya watumiaji yanashughulikiwa.

Picha: Conny Mirbach

Uboreshaji wa usalama mtandaoni

Pata maelezo kuhusu jinsi tunavyohakikisha usalama wa watu wengi zaidi mtandaoni kuliko shirika lolote lingine duniani.

Pata maelezo zaidi