Kituo kimoja cha udhibiti: Akaunti ya Google

Stephan Micklitz na Jan Hannemann wametumia miaka mingi kutengeneza zana ambazo zinawawezesha watumiaji kubainisha data ambayo wangependa kushiriki na Google – na data ambayo hawangependa kuishiriki

Stephan Micklitz anapowaambia watu kuwa anafanya kazi kwenye Google, mara nyingi huulizwa kuwa “kwa nini mnahitaji data nyingi sana?” Jibu lake huwa: “Data inaweza kufanya bidhaa za Google ziwe muhimu zaidi kwako — kama vile kukupa matokeo ya utafutaji kwa lugha sahihi au kukupendekezea njia ya haraka ya kufika nyumbani. Lakini mimi huelezea kila wakati kuwa unaweza kuchagua jinsi Google inavyohifadhi data yako na ikiwa tunaweza kuitumia ili kutengeneza bidhaa zinazokufaa zaidi. Kwa kawaida watu hutaka kujionea hilo wenyewe kabla ya kuniamini!”

"Tulitaka kuweka mapendeleo ya huduma na kufanya muundo ueleweke vizuri zaidi."

Jan Hannemann

Micklitz amefanya kazi katika Google tangu mwaka wa 2007. Alikuwa mmoja wa wafanyakazi wa kwanza jijini Munich na alichukua jukumu la uongozi kwa haraka katika masuala yanayohusiana na usalama wa mtandaoni na faragha ya data. Tangu mwaka wa 2010, Micklitz ameongoza utengenezaji wa jumla wa bidhaa kadhaa muhimu zaidi za Google za kuimarisha faragha na usalama wa mtandaoni. Anaamini kuwa Google ilichukua hatua bora zaidi ya kuweka makao makuu ya idara hii nchini Ujerumani katika mwaka wa 2008. “Google ilitaka kuwa mahali ambapo suala la faragha lilikuwa linajadiliwa kwa kina zaidi,” Micklitz anakumbuka.

Tangu wakati huo, mengi yametendeka. Muhimu zaidi, mnamo tarehe 25 Mei 2018, Sheria ya Jumla ya Ulinzi wa Data ya Umoja wa Ulaya (GDPR) ilianza kutekelezwa. GDPR hudhibiti matumizi na uhifadhi wa data binafsi. Micklitz anakumbuka wakati ambapo yeye na wafanyakazi wenzake walisoma sheria hiyo kwa mara ya kwanza mwaka wa 2016. “Ilikuwa bayana kuwa zana na vidhibiti vingi tulivyokuwa tumeunda vilikuwa tayari vinatii GDPR -- lakini pia kuwa bado tulihitaji kuvishughulikia,” anakumbuka. Sasa, ananipeleka kwenye chumba cha mikutano ambapo anakutana na mfanyakazi mwenzake Jan Hannemann.

Mkurugenzi wa Uhandisi Stephan Micklitz (kushoto) anawajibikia faragha na usalama wa jumla katika Google. Alisomea sayansi ya kompyuta katika Chuo Kikuu cha Kiufundi cha Munich na amefanya kazi katika ofisi ya Google jijini Munich tangu mwishoni mwa mwaka wa 2007.

Google ilianzisha zana yake ya kwanza ya faragha ya data, Dashibodi ya Google, mwaka wa 2009. Micklitz na timu zake waliwajibikia kubuniwa kwa zana hiyo. Baada ya miaka mingi, vipengele vya ziada vimeongezwa. Kuanzia mwaka wa 2013, watumiaji wameweza kudhibiti maelezo yao ya dijitali kwenye Google kwa kutumia Kidhibiti cha Akaunti Isiyotumika; mwaka wa 2014, Ukaguzi wa Usalama uliongezwa, ukifuatwa na Ukaguzi wa Faragha mwaka wa 2015. Zana hizi mpya zinawaelekeza watumiaji kwenye mipangilio ya faragha na usalama wa data yao hatua kwa hatua.

Mwaka wa 2015, Akaunti Yangu ilianzishwa, hatua iliyoleta pamoja huduma zote za Google. Kwa mara ya kwanza, watumiaji walikuwa na kituo kimoja cha udhibiti ambacho kiliwawezesha kuona aina ya data yao binafsi iliyokuwa inahifadhiwa na Google, kubainisha wenyewe taarifa walizotaka kufuta na kuzima vipengele ambavyo huhifadhi data na kufuatilia shughuli za mtandaoni. Watumiaji pia wangeweza kujiondoa ili wasipokee matangazo yaliyowekewa mapendeleo. Akaunti Yangu imeendelea kupanuliwa na kuboreshwa tangu ilipoanzishwa.

"Ni muhimu kwetu kuwa kila mtumiaji anaweza kuchagua taarifa ambazo Google inaruhusiwa kuhifadhi."

Stephan Micklitz

Mnamo Juni 2018, huduma ilitengenezwa upya na Akaunti Yangu ikabadilika kuwa Akaunti ya Google. Pamoja na Stephan Micklitz, Msimamizi wa Bidhaa Jan Hannemann aliwajibikia uzinduzi huo. Hannemann ana shahada ya PhD katika sayansi ya kompyuta na amefanya kazi katika Ofisi ya Google jijini Munich tangu mwaka wa 2013. Alisaidia katika kubuni Akaunti Yangu na anawajibikia Akaunti ya Google kufikia sasa. Wafanyakazi wenzake wamempa jina la utani la “Bw. Akaunti ya Google.”

Hannemann anafafanua muundo mpya wa Akaunti ya Google kwa kutumia simu yake mahiri. “Tulitaka kuweka mapendeleo ya huduma na kufanya muundo ueleweke vizuri zaidi – hasa kwa utumiaji kwenye vifaa vya mkononi vyenye skrini ndogo.” Stephan Micklitz anachukua simu yake mahiri na kufungua programu. “Kwa mfano, ninapoanzisha huduma, programu inanipa chaguo la kutekeleza Ukaguzi wa Usalama,” anaelezea. “Hapa ninaweza kuona mara moja ikiwa Google ina mapendekezo yoyote kuhusu jinsi ninavyoweza kuboresha usalama wa Akaunti yangu ya Google.”

Jan Hannemann (kushoto) ni Msimamizi wa Bidhaa wa Akaunti ya Google, iliyojulikana awali kama Akaunti Yangu. Huduma ni kituo kimoja cha udhibiti kwa watumiaji, ambacho kinawawezesha wakague usalama na faragha ya data yao.

Micklitz na Hannemann huhusisha kazi yao nyingi ya utengenezaji wa bidhaa na utafiti wa Google kuhusu jinsi watu duniani kote hutumia huduma mahususi na hisia zao za jumla kuhusu huduma wanazotumia. Hannemann anasema kuwa “Watu wa Ulaya – Wajerumani hasa – mara nyingi huwa na shaka kuhusiana na suala la matumizi ya data yao binafsi kuliko Wamarekani,”. “Bila shaka, hali hiyo inatokana na historia yetu.” Si watumiaji wote wanaopinga kuhifadhiwa kwa data yao. “Baadhi ya watu huona kuwa ni jambo linalofaa wakati simu zao mahiri zinawakumbusha kuwa ni wakati wa kuelekea kwenye uwanja wa ndege,” anasema Hannemann. “Watu wengine hufurahia kipengele cha kukamilisha kiotomatiki, ambacho huwezesha mtambo wa kutafuta kutabiri maneno yaliyosalia ya hoja ya utafutaji. Vipengele hivi na vingine vingi vinaweza kutumika tu watu wanapoturuhusu tutumie data yao ili kufanya bidhaa zetu ziwafae zaidi.

Stephan Micklitz anasema kuwa suala la faragha haliwezi kushughulikiwa kwa njia moja pekee. Hali hii inatokana kwa kiasi fulani na ukweli kuwa kila mtu ni mahususi na watumiaji wanahitaji mabadiliko baada ya muda fulani. “Ni muhimu kwetu kuwa kila mtumiaji aweza kuchagua maelezo ambayo Google inaruhusiwa kuhifadhi. Tunaendelea kunoa zana zetu ili kufanikisha suala hilo.”

Picha: Conny Mirbach

Uboreshaji wa usalama mtandaoni

Pata maelezo kuhusu jinsi tunavyohakikisha usalama wa watu wengi zaidi mtandaoni kuliko shirika lolote lingine duniani.

Pata maelezo zaidi