Kuvinjari kwa usalama mtandaoni

Lena Rohou kutoka Google anasimamia mpango wa Ujerumani wa Google Digital Garage, ambao ofa zake zinajumuisha kozi za mafunzo katika usalama wa data

Bi. Rohou, ufahamu kuhusu faragha na usalama wa data ni muhimu kwa kampuni na watu binafsi. Mnafunza kozi zipi katika mada hii?

Katika Google Digital Garage, tuna mafunzo katika ujuzi wa dijitali kwa watu ambao wangependa kuendeleza kazi zao wenyewe au kusaidia kukuza kampuni zao. Mada za kozi zinaanzia mambo ya msingi ya utangazaji wa bidhaa dijitali hadi kuongeza tija kazini. Katika kozi zetu kuhusu faragha na usalama wa data, tunaelezea uthibitishaji wa hatua mbili – mchakato wa hatua mbili wa kuingia katika akaunti. Tunaelezea pia maana ya wizi wa data binafsi na jinsi ya kujilinda dhidi ya wizi huo. Wamiliki wa biashara wanaweza kuhudhuria kozi za Digital Garage ili kupata maelezo kuhusu jinsi ya kujumuisha HTTPS kwenye tovuti.

Kozi hufanywa vipi?

Kozi zetu zote hazilipishwi – iwe unajiunga na kozi katika mojawapo ya maeneo yetu ya Munich, Hamburg au Berlin, ama unatumia mfumo wa mtandaoni wa Digital Garage. Kozi za mtandaoni huchukua takribani saa mbili na jambo zuri sana kuhusu kozi hizi ni kwamba zinakupa fursa ya kuzungumza na washiriki wengine na kupata marafiki wapya wanaovutia.

Washiriki hupata ujuzi upi mpya?

Bila shaka, hakuna mtu anayeweza kuwa mtaalamu baada ya saa mbili tu. Lakini ni muda wa kutosha kuelewa mambo ya msingi na kukuza hisia nzuri kuhusu jinsi unavyoweza kukagua ulimwengu dijitali kwa njia salama zaidi, kwa faragha na pia kwa utaalamu.

Jisajili sasa na ujiunge na

Google Digital Garage, ambayo ina kozi zisizolipishwa ili kukutayarisha kwa kizazi cha dijitali. Jikuze au ukuze taaluma yako katika mojawapo wa maeneo ya kozi au ukiwa nyumbani kwako.

Kwa kozi nchini Ujerumani, tembelea zukunftswerkstatt.de

Kwa kozi nchini Uingereza, tembelea learndigital.withgoogle.com/digitalgarage

Kwa kozi nchini Italia, tembelea learndigital.withgoogle.com/digitaltraining

Kwa kozi nchini Ufaransa, tembelea learndigital.withgoogle.com/ateliersnumeriques

Kwa kozi nchini Uhispania, tembelea learndigital.withgoogle.com/activatunegocio

Kwa kozi nchini Uholanzi, tembelea learndigital.withgoogle.com/digitalewerkplaats

Picha: Eva Häberle

Uboreshaji wa usalama mtandaoni

Pata maelezo kuhusu jinsi tunavyohakikisha usalama wa watu wengi zaidi mtandaoni kuliko shirika lolote lingine duniani.

Pata maelezo zaidi