Kusaidia kufanya
mazingira ya mtandaoni kuwa salama zaidi.

Kufanya teknolojia imfae kila mtu kunamaanisha kulinda kila mtu anayeitumia. Tumejitolea kubuni na kushiriki teknolojia za faragha na usalama ambazo zinalinda watumiaji wetu na kukuza sekta.

Video inayoweza kuchezwa kuhusu Faragha kwenye programu ya Mratibu wa Google
Kuvumbua ili kulinda
usalama wa watumiaji wetu mtandaoni.

Kadri hatari mpya zinavyoibuka na mahitaji ya watumiaji kubadilika, ndivyo tunavyoendelea kuvumbua ili kulinda kiotomatiki taarifa za faragha za kila mtumiaji, katika kila kiwango cha hatari, kwenye bidhaa zetu zote.

Simu inayoangazia mtu akiandika "he" na Google ikitabiri kiotomatiki neno "Hey"

Mafunzo Shirikishi

Kubuni bidhaa muhimu kwa kutumia data chache

Mafunzo shirikishi ni teknolojia ya kupunguza data iliyoanzishwa katika Google ambayo inaleta teknolojia ya mashine kujifunza (ML) moja kwa moja kwenye kifaa chako. Mbinu hii mpya huweka pamoja taarifa ambazo utambulisho wake umefichwa kutoka kwenye vifaa mbalimbali ili kufunza miundo ya ML. Mafunzo shirikishi husaidia kulinda faragha yako kwa kuhifadhi taarifa binafsi nyingi iwezekanavyo kwenye kifaa chako.

Mpango wa Ulinzi wa Hali ya Juu

Ulinzi thabiti zaidi wa Google, kwa watu wanaouhitaji zaidi

Mpango wa Ulinzi wa Hali ya Juu hulinda Akaunti za Google za binafsi za walio katika hatari kubwa ya kulengwa na mashambulizi mahususi ya mtandaoni – kama vile wanahabari, wanaharakati, viongozi wa kibiashara na timu za kampeni za kisiasa. Mpango huu hutoa ulinzi wa kina wa akaunti dhidi ya aina nyingi za hatari na huendelea kubadilika ili kuongeza mbinu mpya za ulinzi.

Kuboresha viwango vya sekta
ili kufanya intaneti iwe
salama kwa kila mtu.

Tunataka kuwalinda watumiaji wetu kila wakiwa mtandaoni kwa kuimarisha usalama wa mtandao wote wa intaneti, si tu kwa huduma na bidhaa za Google. Teknolojia tunazounda kwa ajili ya usalama na faragha ni miongoni mwa zilizo madhubuti zaidi duniani na tunazishiriki waziwazi ili wengine waweze kuzitumia.

Simu inayoonyesha arifa kuwa muunganisho ni salama

Usimbaji fiche wa HTTPS

Kusaidia kulinda usalama wa tovuti kwenye wavuti zote kupitia mbinu za kina za usimbaji fiche

Kutumia usimbaji fiche wa HTTPS kwenye huduma zetu huhakikisha kuwa unaweza kuunganisha kwenye tovuti kwa njia salama na uweke taarifa zako za faragha kama vile nambari ya kadi ya mikopo, bila mtu yeyote kuiba taarifa hizo. Tutaendelea kuwekeza ili kuhakikisha kuwa huduma na tovuti zetu zinatoa usimbaji fiche wa HTTPS kwa chaguomsingi na tutasaidia wavuti zilizosalia pia kuanza kutumia usimbaji fiche wa HTTPS kwa kutoa zana na nyenzo kwa wasanidi programu wote.

Faragha kwa Kuchanganya Data

Kusaidia mashirika yafiche utambulisho wa data kwa kutumia mbinu ya faragha kwa kuchanganya data

Faragha kwa kuchanganya data ni teknolojia ya kina ya kuficha utambulisho wa data ambayo inatuwezesha kupata maarifa kutoka kwenye data bila kuathiri ufiche wa utambulisho wa data ya watumiaji wetu. Tumetumia zaidi ya mwongo mmoja kubuni maktaba kubwa zaidi ya algoriti za faragha kwa kuchanganya data duniani na tumetengeneza programu huria ya maktaba hii ili kusaidia mashirika yatumie kwa urahisi ulinzi sawa wa faragha kwenye data yao.

Kituo cha Uhandisi wa Usalama kwenye Google
Kubuni mustakabali
wa usalama wa mtandaoni.

Chini ya uongozi wa timu ya wahandisi wenye uzoefu, Kituo cha Uhandisi wa Usalama kwenye Google ni kitovu kikuu cha kazi za usalama wa intaneti katika Google. Kwa kuelewa tatizo, kubuni suluhisho, kushirikiana na wengine na kuhamasisha watumiaji kila mahali, tunaweza kubuni intaneti iliyo bora na salama kwa kila mtu.

Pata maelezo zaidi

Gundua jinsi Google husaidia
kulinda kila mtu mtandaoni.