Kukuza viwango vya sekta
ili kufanya intaneti
iwe salama kwa kila mtu.

Usalama na faragha ya watumiaji wetu ndilo jambo la msingi tunalofanya katika kila bidhaa tunayobuni. Tunaongoza sekta katika kubuni na kushiriki teknolojia za usalama ambazo hukuza viwango vya sekta kwa kila mtu.

Kuvumbua ili
kulinda watumiaji mtandaoni.

Kadri hatari mpya zinavyoibuka na mahitaji ya watumiaji kubadilika, ndivyo tunavyoendelea kuvumbua ili kulinda kiotomatiki taarifa za faragha za kila mtumiaji, katika kila kiwango cha hatari, kwenye bidhaa zetu zote.

Mpango wa Ulinzi wa Hali ya Juu

Usalama thabiti zaidi wa Google,
kwa wanaouhitaji zaidi

Mpango wa Ulinzi wa Hali ya Juu ndicho kipengele thabiti zaidi cha usalama wa akaunti kwenye Google na mpango wa kwanza wa sekta ambao umebuniwa kulinda Akaunti za Google za binafsi na za biashara za walio katika hatari ya kushambuliwa mtandaoni – kama vile watunzi wa sera, timu za kampeni, wanahabari, wanaharakati na viongozi wa biashara. Mpango huu hutoa ulinzi wa kina wa akaunti dhidi ya aina nyingi za hatari na huendelea kubadilika ili kuongeza mbinu mpya za ulinzi.

Gundua Mpango wa Ulinzi wa Hali ya Juu

KUPUNGUZA DATA

Kudhibiti taarifa binafsi zinazotumiwa na kuhifadhiwa

Tunaamini bidhaa zinapaswa tu kuhifadhi taarifa zako kwa muda ambao unakufaa – iwe ni kuweza kupata maeneo unayopenda kwenye Ramani au kupata mapendekezo ya mambo ya kutazama kwenye YouTube.

Mara ya kwanza unapowasha Kumbukumbu ya Maeneo Yangu – ambayo huwa imezimwa kwa chaguomsingi – chaguo lako la kufuta kiotomatiki litawekwa kuwa miezi 18 kwa chaguomsingi. Kufuta kiotomatiki Historia ya Shughuli kwenye Wavuti na Programu kutakuwa pia miezi 18 kwa chaguomsingi katika akaunti mpya. Hii inamaanisha kuwa data ya shughuli zako itafutwa kiotomatiki na kila mara baada ya miezi 18, badala ya kuhifadhiwa hadi utakapochagua kuifuta. Unaweza kuzima mipangilio hii au kubadilisha mipangilio ya kufuta kiotomatiki wakati wowote.

Simu inayoangazia mtu akiandika "he" na Google ikitabiri kiotomatiki neno "Hey"

Mafunzo Shirikishi

Kubuni bidhaa muhimu kwa kutumia data chache

Mafunzo shirikishi ni teknolojia ya kupunguza data iliyoanzishwa katika Google ambayo inaleta teknolojia ya mashine kujifunza (ML) moja kwa moja kwenye kifaa chako. Mbinu hii mpya huweka pamoja taarifa ambazo utambulisho wake umefichwa kutoka kwenye vifaa mbalimbali ili kufunza miundo ya ML. Mafunzo shirikishi husaidia kulinda faragha yako kwa kuhifadhi taarifa binafsi nyingi iwezekanavyo kwenye kifaa chako.

Kuficha Utambulisho wa Data

Kuboresha ulinzi wa faragha kwa kuficha utambulisho wa data

Tunatumia mbinu maarufu za kuficha utambulisho wa data ili kulinda data yako huku tukiboresha huduma zetu zikufae zaidi. Kwa mfano, tunajumlisha data kutoka kwa mamilioni ya watumiaji na tunaficha utambulisho wa data hizo ili uweze kuona jinsi eneo litakuwa na shughuli nyingi kabla ufike huko.

Kipengele cha kuvinjari salama kilichoboreshwa

Kukulinda unapovinjari

Kipengele cha Kuvinjari Salama Kilichoboreshwa kina matumizi zaidi ya ulinzi wetu wa Kuvinjari Salama ili kiwe hima na kikufae zaidi. Kwa wale wanaochagua kuwasha Kipengele cha Kuvinjari Salama Kilichoboreshwa kwenye Chrome, Google itakagua kiotomatiki mwonekano wote wa hatari unazopata kwenye wavuti na mashambulizi dhidi ya Akaunti yako ya Google ili kutoa ulinzi hima na unaofaa dhidi ya wizi wa data binafsi, programu hasidi na vitisho vingine vilivyo kwenye wavuti. Pata maelezo zaidi kuhusu Kipengele cha Kuvinjari Salama Kilichoboreshwa.

Kulinda kila mtu
mtandaoni
kwa kushirikiana.

Tumejitolea kufanya wavuti uwe sehemu salama kwa kila mtu. Ili kusaidia kutimiza hili, tunafanya teknolojia zetu ziwe huria na kufanyanyenzo zetu ziweze kufikiwa na wasanidi programu na mashirika.

Simu inayoangazia arifa kuwa muunganisho ni salama

Usimbaji fiche wa HTTPS

Kusaidia kulinda tovuti kwenye wavuti kupitia usimbaji fiche

Kutumia usimbaji fiche wa HTTPS kwenye huduma zetu huhakikisha kuwa unaweza kuunganisha kwenye tovuti kwa njia salama na uweke taarifa zako za faragha kama vile nambari ya kadi ya mikopo, bila mtu yeyote kuiba taarifa hizo. Tutaendelea kuwekeza ili kuhakikisha kuwa huduma na tovuti zetu zinatoa usimbaji fiche wa HTTPS kwa chaguomsingi na tutasaidia sehemu iliyosaia ya wavuti pia kuanza kutumia usimbaji fiche wa HTTPS kwa kutoa zana na nyenzo kwa wasanidi programu wote.

Simu inayoangazia arifa ya onyo kutoka Google Chrome kuhusu tovuti inayopotosha

Kuvinjari Salama

Kukulinda dhidi ya tovuti, programu na matangazo hatari kwenye wavuti

Tulibuni teknolojia yetu ya Kuvinjari Salama ili kulinda watumiaji wa wavuti dhidi ya programu hasidi na majaribio ya wizi wa data binafsi kwa kuwaarifu watumiaji wanapojaribu kutembelea tovuti hatari. Teknolojia ya Kuvinjari Salama hulinda watumiaji wa Chrome na wengine - ili kufanya intaneti iwe salama na yenye manufaa kwa kila mtu, tuliruhusu kampuni nyingine zitumie teknolojia hii katika vivinjari vyao, ikiwa ni pamoja na Safari ya Apple na Firefox ya Mozilla bila malipo. Kufikia leo, zaidi ya vifaa bilioni 4 vinalindwa kwa teknolojia ya Kuvinjari Salama. Tunatahadharisha pia wamiliki wa tovuti wakati tovuti zao zina hitilafu za kiusalama na kuwapa zana za kuwasaidia kusuluhisha hitilafu hizo bila malipo.

Simu inayoonyesha uwakilishaji wa takwimu za COVID-19

Ripoti ya Google ya Matembezi ya Jamii inayohusiana na COVID-19 hutumia teknolojia ya kiwango cha kimataifa ya kuficha utambulisho wa data, ikiwa ni pamoja na faragha kwa kuchanganya data, ili kuhifadhi data ya watumiaji kwa usalama na faragha.

teknolojia huria za faragha

Kushiriki ulinzi wa faragha na uvumbuzi wetu

Tumejitolea kuendelea kuboresha ulinzi wa faragha tunaotoa na kushiriki maboresho haya na wengine. Ndiyo maana tunatumia kwa njia huria teknolojia zetu kuu za kuficha utambulisho wa data na kupunguza data, kama vile faragha kwa kuchanganya data, mafunzo shirikishi na Private Join and Compute. Tunatumai kuwa zana hizi huria zitasaidia kubuni maarifa ambayo yanafaa kila mtu huku zikiendelea kulinda faragha ya mtu binafsi.

Ulinzi wa akaunti katika huduma nyinginezo
Kupanua ulinzi nje ya Akaunti yako ya Google

Ulinzi wa Akaunti katika Huduma Nyinginezo hupanua usalama ulio kwenye Akaunti yako ya Google ili ufikie programu na tovuti ambazo unaingia ukitumia Google. Programu na tovuti zikiwa zimetekeleza Ulinzi wa Akaunti katika Huduma Nyinginezo, tunaweza kutuma maelezo kuhusu matukio ya usalama – kwa mfano, utekaji wa akaunti – ili programu na tovuti hizo pia ziweze kukulinda. Ili kubuni teknolojia hii inayoongoza, tumefanya kazi na kampuni kuu za teknoloja na jumuiya ya viwango ili kurahisishia programu zote kutekeleza.

Zawadi za ulinzi
Kuhimiza washirika wa sekta kufumbua hatari za kiusalama

Katika Google, tulianzisha mipango ya zawadi za ulinzi zinazotolewa kwa watafiti huru ili watambue uwezekano wa hatari katika huduma zetu. Ili kutuza michango bora ya watafiti huru ambayo inatusaidia kulinda watumiaji wetu, tunatoa mamilioni ya dola katika ruzuku za utafiti na utafutaji wa hitilafu kila mwaka. Kwa sasa, tunatoa zawadi za ulinzi katika bidhaa zetu nyingi zikiwemo Chrome na Android.

Mbali na kushirikisha watafiti huru, pia tuna timu ya ndani ya wahandisi inayojulikana kama Project Zero, ambayo hufuatilia na kushugulikia hitilafu za usalama katika programu zinazotumiwa kote kwenye intaneti.

Viwango vya uthibitishaji
Kuboresha viwango vya uthibitishaji ili kukulinda

Tumekuwa tukiongoza katika kubuni au kutumia viwango thabiti zaidi vya uthibitishaji na kuingia katika akaunti kwenye wavuti. Tunashirikiana na wadau wote wa sekta na kushiriki teknolojia kwa kubuni viwango vya pamoja kwa ajili ya wavuti. Kwa mfano, tumeshirikiana na shirika lisilo la faida la FIDO Alliance ili kubuni na kutumia viwango vipya vya sekta kwa watumiaji, kampuni na wafanyakazi wao kutumia, hali inayohakikisha ufikiaji salama wa akaunti kwa kila mtu.

Usalama huria
Kuwapa wasanidi programu zana za usalama ili waweze kusaidia kupunguza hatari za kiusalama

Tunashiriki teknolojia yetu ya usalama wakati wowote tunapoamini kuwa inaweza kuwafaa wengine. Kwa mfano, tunawapa wasanidi programu Kichanganuzi cha Usalama wa Wavuti kwenye Wingu la Google bila malipo ili waweze kuchanganua programu zao za wavuti ili kubaini hatari za kiusalama. Tumechangia zana nyingi za usalama, zilizobuniwa ndani ya kampuni, kuwa miradi huria ili wengine watumie.

Wataalamu wa Google wa Usalama na Imani wakishiriki vidokezo vya faragha na usalama katika Federal Triangle jijini Washington, DC.

Mafunzo ya usalama mtandaoni
Kutoa mafunzo kuhusu usambazaji na usalama mtandaoni ili kudumisha usalama bora kwa wote

Tunatoa nyenzo za kielimu, mafunzo na zana ili kusaidia watu kote duniani kupata maelezo kuhusu jinsi ya kuwa salama mtandaoni. Kila mwaka, timu yetu ya mafunzo hufikia zaidi ya watu milioni 100 - wakiwemo waelimishaji, wanafunzi, wazazi, wakongwe na watu walio na ulemavu – kupitia nyenzo na mafunzo ya usalama mtandaoni.

Project Shield
Kulinda tovuti za habari zisizimwe

Project Shield ni huduma inayotumia teknolojia yetu ya usalama ili kusaidia kulinda habari, mashirika ya haki za binadamu, tovuti za kupiga kura, mashirika ya kisiasa na kampeni na wagombeaji dhidi ya mashambulizi yanayosambazwa ya kuzuia huduma (DDoS). Mashambulizi haya ni majaribio ya kufanya tovuti ziache kufanya kazi kwa kuzitumia data nyingi bandia, hivyo kuzuia watumiaji wasifikie maelezo muhimu. Licha ya ukubwa wa tovuti au ukubwa wa shambulizi, Project Shield hailipishwi kamwe.

Uwezo wa kubeba data
Uvumbuzi maarufu zaidi wa faragha na usalama katika uwezo wa kubeba data

Tumezindua mfumo huria wa kubeba data na tunaendelea kushirikiana na kampuni kama vile Apple, Microsoft, Facebook na Twitter ili kuwasaidia watu kuhamisha data yao kwenye wavuti na kujaribu kwa urahisi watoa huduma wapya mtandaoni.

Ushirikiano wa faragha
Kubuni wavuti wenye faragha zaidi kwa kila mtu

Tumejitolea kubuni fursa za kushirikisha kama vile Sehemu ya Majaribio ya Faragha na kufanya kazi na jumuiya ya wavutini ili kubuni kundi la viwango huria vinavyolinda faragha ya watumiaji huku vikiendelea kutoa maudhui yanayoweza kufikiwa kwenye wavuti bila malipo. Kwa kushiriki nyenzo na mifumo yetu, tunatumai kupiga hatua za kuelekea kwenye wavuti wenye faragha zaidi.

Kufuatilia waliotangamana na aliyeambukizwa

Tunalinda faragha ya watumiaji huku tukisaidia mamlaka
za afya ya umma kukabili COVID-19

Ili kusaidia serikali kukabili janga la COVID-19, Google na Apple kwa pamoja zilibuni teknolojia za kufuatilia waliotangamana na aliyeambukizwa kama vile Mfumo wa Arifa Kuhusu Kukaribia Aliye na COVID-19 huku masuala ya faragha na usalama yakipewa kipaumbele. Kwa kushirikiana kwa karibu na wasanidi programu, serikali na watoa huduma za afya ya umma, tunatazamia kubuni teknolojia ili kuendelea kusuluhisha masuala ya dunia huku tukiendelea kulinda viwango vya juu vya faragha ya watumiaji.

Kituo cha Uhandisi

Pata maelezo kuhusu jinsi Kituo cha Uhandisi wa Usalama kwenye Google kinavyobuni teknolojia kwa ajili ya usalama wa mtandaoni kwa kuangazia siku za usoni.