Njia salama ya kutafuta

Zaidi ya miaka 20 iliyopita, mabilioni ya watu wameamini Tafuta na Google katika maswali yao. Kila siku tunafanya kazi kuaminiwa kutoa taarifa ya kuaminika na kulinda faragha yako kwa kutumia teknolojia ya usalama iliyojumuishwa.

Muundo wa Utafutaji ni wa faragha

Tunalinda data yako kwa kutumia teknolojia bora zaidi katika sekta na kusimba utafutaji wote kwa njia fiche. Tukuundia vidhibiti ili uweze kuchagua mpangilio wa faragha inayokufaa. Na hatuuzi kamwe taarifa zako za binafsi.

Usalama wa Data

Ili kulinda data yako, tumeunda baadhi ya miundombinu bora zaidi kwa usalama duniani. Miundombinu hii inahifadhi data yako kwa faragha na kwa usalama inapohamishwa kutoka kwenye kifaa chako hadi kwenye vituo vyetu vya data. Ikiwa utahifadhi historia yako ya Utafutaji kwenye akaunti yako ya Google, data unayotengeneza inazunguka kati ya kifaa chako, huduma za Google, na vituo vyetu vya data. Tunalinda data hii kupitia safu nyingi za usalama, ikiwa ni pamoja na teknolojia bora ya usimbaji fiche kama HTTPS na usimbaji fiche wote.

Uwajibikiaji Data

Tuna wajibu wa kulinda na kuheshimu data yako. Hii ndiyo sababu hatuuzi kamwe taarifa zako za binafsi.

Vidhibiti-rahisi-kutumia

Utafutaji una vithibiti vya faragha ili uweze kuchagua kile utahifadhi kwenye Akaunti yako ya Google . Pia unaweza kuwasha kipengele cha kufuta-kiotomatiki ili kufuta kiotomatiki data yako mara kwa mara.

Ulinzi wa faragha katika historia yako ya Utafutaji

Ikiwa unashiriki kifaa, unaweza kuhitaji kuhakikisha kwamba watu wengine wanaoitumia hawawezi kufika Shughuli Yangu na kutazama historia za Utafutaji zilizohifadhiwa hapo. Sasa unaweza kuchagua kuhitaji uthibitishaji wa ziada kwa Shughuli Yangu. Katika mpangilio huu, utahitaji kutoa taarifa za ziada — kama vile nenosiri lako au uthibitishaji wa hatua-mbili — kabla ya historia yako kamili kutazamwa.

Google inakulinda wakati unapofanya utafutaji

Tafuta na Google ni njia salama zaidi ya kutafuta. Kila siku Utafutaji unazuia tovuti za barua taka bilioni 40 kutoka kwa matokea ya utafutaji ili uweze kutafuta kwa usalama, na kukulinda kiamilifu kwa kusimba kwa njia fiche utafutaji wako wote. Utafutaji pia una zana za kujifunza zaidi kuhusu matokeo yako na kudhibiti hali yako ya Utafutaji.

Utafutaji unazuia mapema barua taka mtandaoni kuonekana kwenye matokeo

Utafutaji unazuia mapema barua taka mtandaoni kuonekana kwenye matokeo

Utafutaji unakusaidia kukulinda dhidi ya tovuti hasidi ambapo taarifa binafsi au utambulisho wako unaweza kuibwa. Kila siku tunagundua na kuzuia kurasa bilioni 40 za barua taka kutoka kwenye matokeo ya utafutaji - ikiwa ni pamoja na tovuti ambazo zina programu hasidi au zilizoundwa kwa udanganyifu kuiba taarifa zako binafsi.

Kipengele cha Kuvinjari kwa Usalama

Kipengele cha Kuvinjari kwa Usalama

Google Kipengele cha Kuvinjari kwa Usalama kinalinda zaidi ya vifaa bilioni nne na, wakati kimewashwa kwenye Chrome, huonyesha ujumbe wa onyo ili kukujulisha kwamba tovuti unayojaribu kuingia huenda salama. Maonyo haya yanasaidia kukulinda na kulinda taarifa zako binafsi dhidi ya programu hasidi na ulaghahi wa kuhadaa.

Utafutaji wote unalindwa kwa usimbaji fiche

Utafutaji wote kwenye Google.com na katika programu ya Google uasimbwa kwa njia fiche kwa chaguomsingi, ili kulinda taarifa zako salama kutokana na mtu yeyote anayejaribu kuiba data.

Utafutaji Salama

Utafutaji Salama umeundwa kugundua maudhui chafu kama vile ponografia au picha zinazoonyesha vurugu kwenye Utafutaji wa Google. Ikiwa hungependa kuona maudhui machafu kwenye matokeo yako ya utafutaji, unaweza kuchagua Chuja kuzuia maudhui yoyote machafu ambayo yamegunduliwa, au Kipengele cha ukungu ili kuweka ukungu kwenye picha chafu.

Utafutaji Salama umeundwa Kuchuja kiotomatiki wakati mifumo ya Google inaonyesha kwamba huenda una umri wa chini ya miaka 18.

Ni rahisi kufuta historia ya Utafutaji kutoka kwenye akaunti yako - au kuchagua kutohifadhi kabisa

Ni rahisi kudhibiti jinsi unavyotaka historia yako ya Utafutaji kuhifadhiwa kwenye akaunti yako ya Google — ikiwemo ikiwa hungependa kuihifadhi kamwe.

Kufuta historia yako ya Utafutaji katika Shughuli Yangu

Wakati unapotafuta kwenye Google kama Shughuli ya Tovuti Programu imewashwa, Google huhifadhi shughuli kama historia yako ya Utafutaji katika Akaunti yako ya Google. Tunatumia shughuli zako zilizohifadhiwa katika huduma zote za Google kukupa hali ya utumiaji iliyobinafsishwa zaidi, kama vile mapendekezo na maudhui ya programu. Unaweza kwenda kwenye Shughuli Yangu kufuta baadhi au historia zote za Utafutaji zilizohifadhiwa katika Akaunti yako ya Google na kudhibiti mipangilio kama vile aina ya shughuli ambayo Google inahifadhi na wakati ambapo Google inafuta kiotomatiki shughuli yako iliyohifadhiwa.

Kumbuka kwamba hata kama historia yako ya Utafutaji haijahifadhiwa katika Akaunti yako ya Google, au uliifuta kutoka kwenye Shughuli yangu, kivinjari chako kinaweza bado kuihifadhi. Angalia maagizo ya kivinjari chako kwa maagizo kuhusu jinsi ya kufuta historia yako ya kivinjari.

Tumia vidhibiti vya kufuta kiotomatiki

Tumia vidhibiti vya kufuta kiotomatiki

Unaweza kuchagua kufanya Google kufuta historia yako ya Utafutaji kiotomatiki na kufuta historia yako ya Utafutaji mara kwa mara, pamoja na Shughuli zingine za Tovuti na Programu, kutoka kwa akaunti yako baada ya miezi mitatu, 18 au 36. Kwa akaunti mpya, chaguomsingi ya kufuta kiotomatiki Shughuli ya Tovuti na Programu ni miezi 18, lakini bado unaweza kubadilisha mipangilio yako ukitaka.

Pata maelezo zaidi kuhusu
Tafuta na Google
Pata maelezo kuhusu jinsi usalama unavyojumuishwa kwenye
kila bidhaa tunayobuni.