Mahali salama
pa kuweka kumbukumbu za maisha.

Programu ya Picha kwenye Google ni mahali ambako picha na video zako zote huhifadhiwa, kupangwa kiotomatiki na kutumiwa kwa urahisi. Tunawekeza kwenye mifumo bora zaidi ya usalama na vidhibiti vya faragha ambavyo ni rahisi kutumiwa ili uweze kuhifadhi na kushiriki kumbukumbu zako kwa usalama.

Njia zote ambazo programu ya Picha kwenye Google husaidia kulinda usalama wa kumbukumbu zako.
Kulinda usalama wa kumbukumbu
Tunaendesha mojawapo ya mifumo bora zaidi ya usalama, iliyo na kila kitu kuanzia kwa vituo vya data vilivyobuniwa kwa njia maalum hadi mikongo ya kimataifa ya mawasiliano ambayo huchunguzwa mara kwa mara ili kusaidia kulinda usalama wa kumbukumbu zako.

Hifadhi salama

Huduma za Google huendelea kulindwa na mfumo wa kina zaidi wa usalama kote duniani. Usalama huu uliojumuishwa hutambua na kuzuia hatari za mtandaoni ili uwe na uhakika kuwa taarifa zako binafsi ni salama.

Usimbaji fiche

Usimbaji fiche hudumisha usalama na faragha ya data inapotumwa. Unapohifadhi picha, data unayotengeneza huhamishwa kati ya kifaa chako, huduma za Google na vituo vyetu vya data. Tunalinda data hii kwa kutumia safu nyingi za usalama, ikiwa ni pamoja na teknolojia bora zaidi ya usimbaji fiche kama vile HTTPS na usimbaji wakati data imehifadhiwa.

Kushughulikia data kwa kuwajibika
Watu hutumia picha zao kwenye vifaa na programu mbalimbali. Tunapojitahidi kukurahisishia kufanya mambo mengi kwa kutumia picha unazopiga, matukio haya ya kurahisisha mambo yanapaswa kutumiwa kwa uwajibikaji kwenye programu zingine zaidi ya programu ya Picha kwenye Google na hali ya utumiaji wa wavuti.

Kupanga picha katika makundi kulingana na nyuso za waliomo

Kipengele cha kupanga picha kulingana na nyuso za waliomo huweka kiotomatiki nyuso zinazofanana kwenye kikundi na kukupangia ili kukurahisishia kutafuta na kudhibiti picha zako. Ni wewe tu unayeweza kuona lebo na makundi ya nyuso. Unaweza kudhibiti ikiwa kipengele cha kupanga picha kulingana na nyuso za waliomo kimezimwa au kimewashwa na ukikizima, makundi ya nyuso yatafutwa kwenye akaunti yako. Hatubuni teknolojia yenye madhumuni ya jumla ya utambuzi wa sura kwa lengo la kibiashara. Pata maelezo zaidi.

Mpango wa Washirika

Tunashirikiana kwa karibu sana na washirika na wasanidi programu ambao hutumia API ya programu ya Picha kwenye Google ili kuhakikisha kuwa wanabuni vipengele muhimu ambavyo vinaimarisha hali yako ya utumiaji wa programu ya Picha kwenye Google. Washirika wetu wanahitajika kutii sera zetu na hawawezi kufikia data yoyote bila ruhusa yako.

Kukupa uwezo wa kudhibiti
Data hufanya programu ya Picha kwenye Google iwe muhimu na ifae zaidi, lakini tungependa kukusaidia uwe na uwezo wa kudhibiti hali yako ya utumiaji. Tumejumuisha zana ambazo ni rahisi kutumia kwenye bidhaa yetu. Zana hizi hukupa uwezo wa kudhibiti na kukuwezesha uchague mipangilio inayokufaa.

Hali maalum ya kuhifadhi nakala

Unaweza kuchagua kuhifadhi nakala ya picha na video zako kwenye programu ya Picha kwenye Google au uhifadhi tu nakala za picha ambazo ungependa kuhifadhi kwenye akaunti yako ya Google.

Kumbukumbu

Furahia kumbukumbu zako bora, unazoonyeshwa kwa faragha. Una chaguo la kujiondoa ili usione Kumbukumbu za watu au vipindi fulani, pia una uwezo wa kufunga kipengele hiki.

Mwonekano wa Ramani

Angalia picha zako kulingana na mahali kwenye ramani wasilianifu ambayo ni wewe tu unayeweza kuiona. Mwonekano huu wa ramani huwekwa kwa kutumia data ya mahali iliyohifadhiwa kwenye Akaunti yako ya Google. Unaweza kubadilisha na kuondoa data ya mahali inayotumiwa kuweka ramani katika photos.google.com. Kama hungependa kuona picha zako za baadaye zikiwa zimepangwa kwenye mwonekano huu wa ramani, unaweza kuzima mipangilio ya Kumbukumbu ya Maeneo Yangu na data ya mahali kwenye programu yako ya kamera.

Mratibu wa Google

Uliza programu ya Mratibu wa Google ili ikusaidie upate, uangalie au ushiriki picha. Kwenye mipangilio yako ya programu ya Mratibu, unaweza kuchagua unachotaka kuonyesha na kushiriki kutoka kwenye vifaa vyako vilivyo na programu ya Mratibu, kama vile Google Nest Hub au simu yoyote ya Android. Ili uratibu na kudhibiti picha zinazoonekana kwenye Skrini Mahiri mahususi au vifaa vya kutuma maudhui vilivyounganishwa, unaweza kutumia mipangilio ya kifaa mahususi kwenye programu yako ya Google Home.

Kushiriki kwa njia salama
Iwe ni picha moja au albamu yote, unaweza kudhibiti unayeshiriki naye kumbukumbu zako. Vidhibiti rahisi na salama vinakuwezesha ushiriki maudhui yako na watu mahususi au unaweza kutumia kiungo kinachoweza kushirikiwa ili uyashiriki kwa wingi.

Kushiriki albamu

Unaposhiriki albamu, mipangilio chaguomsingi itakuwa ni kushiriki na watu au mtu mahususi kupitia Akaunti yake ya Google. Hatua hii inakupatia uwezo zaidi wa kudhibiti anayeweza kuongezwa kwenye albamu. Bado una chaguo la kushiriki kupitia kiungo, hali ambayo inarahisisha shughuli ya kushiriki picha na watu ambao hawatumii programu ya Picha kwenye Google wala Akaunti ya Google. Unaweza kusasisha mipangilio ya kushiriki albamu zako wakati wowote na kudhibiti anayeweza kufikia kila albamu.

Kushiriki moja kwa moja

Unaposhiriki picha na video za mara moja, utakuwa na chaguo la kuziongeza kwenye mazungumzo ya faragha yanayoendelea kwenye programu.

Shughuli za kushiriki

Kila kitu ambacho umeshiriki kupitia programu ya Picha kwenye Google kinapatikana mahali pamoja ili uweze kupata picha zote ambazo umeshiriki na familia na marafiki zako.

Linda picha zako kwa kutumia nafasi ya hifadhi isiyolipishwa katika programu ya Picha kwenye Google.
Gundua
programu ya Picha kwenye Google.
Pata maelezo kuhusu jinsi usalama hujumuishwa kwenye
kila bidhaa tunayotengeneza.