NCMEC, Google na Teknolojia ya Upunguzaji maudhui ya Picha
Nchini Marekani, Kituo cha Kitaifa cha Watoto Waliopotea na Wanaonyanyaswa (NCMEC) hupokea mamilioni ya ripoti za maudhui yanayoonyesha unyanyasaji wa watoto kingono (CSAM) mtandaoni kila mwaka. Makamu wa Rais Mwandamizi na Afisa Mkuu wa Uendeshaji, Michelle DeLaune wa kituo hicho (NCMEC), anazungumzia juu ya maendeleo ya shirika hilo, jinsi kampuni za teknolojia zinavyochukua hatua ya kukabiliana na Maudhui yanayoonyesha unyanyasaji wa watoto kingono (CSAM) na API ya Google ya Ulinganishaji Kiwakilishi.
Je, unaweza kutueleza kuhusu Kituo cha Kitaifa cha Watoto Waliopotea na Wanaonyanyaswa (NCMEC) na jukumu lako ni lipi?
Nimekuwa katika Kituo cha Kitaifa cha Watoto Waliopotea na Wanaonyanyaswa (NCMEC) kwa zaidi ya miaka 20, kwa hiyo nimeshuhudia mabadiliko ya kwanza ya shirika, changamoto na vitisho kwa watoto wetu na usalama wao. Nilianza kufanya kazi hapa kama mchambuzi wa mfumo wa CyberTipline.
Mfumo wa CyberTipline uliundwa na kuzinduliwa mnamo mwaka 1998 kama njia ya wanajumuiya kuripoti matukio ya uwezekano wa unyanyasaji wa watoto. Wakati huo tulikuwa tunapokea ripoti kutoka kwa wazazi ambao walikuwa na wasiwasi kwamba mtu mzima alikuwa akizungumza isivyofaa na mtoto wao mtandaoni na pia watu waliopata tovuti zenye Maudhui yanayoonyesha unyanyasaji wa watoto kingono (CSAM). Kisha sheria ya serikali ilipitishwa nchini Marekani iliyozihitaji kampuni za teknolojia kuripoti kwenye mfumo wa CyberTipline matukio yoyote dhahiri ya Maudhui yanayoonyesha unyanyasaji wa watoto kingono (CSAM) kwenye mifumo yao.
Katika siku za mwanzo, tuliweza kupokea zaidi ya ripoti 100 za unyanyasaji wa watoto kwa wiki. Tulipokea ripoti yetu ya kwanza kutoka katika kampuni ya teknolojia mnamo mwaka 2001. Kufikia mwaka 2021, tunapokea takriban ripoti mpya 70,000 kila siku. Baadhi ya ripoti hizi zinatoka kwa umma, lakini ripoti zetu nyingi zinawasilishwa na kampuni za teknolojia.
Je, Kituo cha Kitaifa cha Watoto Waliopotea na Wanaonyanyaswa (NCMEC) husaidia kwa namna gani kampuni za mtandaoni kukabiliana na Maudhui yanayoonyesha unyanyasaji wa watoto kingono (CSAM)?
Sheria haihitaji kuwepo kwa juhudi zozote za hima zinazofanywa na kampuni. Lakini tu, iwapo kampuni zitagundua au kutambua Maudhui yanayoonyesha unyanyasaji wa watoto kingono (CSAM) lazima zitoe ripoti kuhusu maudhui hayo. Hicho ndio kichocheo kikubwa cha ukuaji muhimu ambao tumeona katika mfumo wa CyberTipline kwa miaka mingi. Lakini katika kipindi cha miaka mitano iliyopita kumekuwa na ongezeko kubwa zaidi la ripoti. Ongezeko hilo linaweza kuhusishwa na juhudi ambazo kampuni nyingi za teknolojia zinachukua kwa hiari kugundua, kuondoa, na kuripoti Maudhui yanayoonyesha unyanyasaji wa watoto kingono (CSAM).
Mojawapo ya programu kubwa zaidi tunazofanyia kazi katika Kituo cha Kitaifa cha Watoto Waliopotea na Wanaonyanyaswa (NCMEC) ni mifumo ya kushiriki kiwakilishi kifupi ili kuwezesha makampuni kuchangia, na nyinginezo kwa ajili ya mashirika yasiyo ya serikali (NGO). Kupitia mfumo wa shirika lisilo la serikali (NGO) wa kushiriki kiwakilishi kifupi, Kituo cha Kitaifa cha Watoto Waliopotea na Wanaonyanyaswa (NCMEC) huzipatia kampuni za teknolojia viwakilishi vifupi zaidi ya milioni tano vya Maudhui yaliyothibitishwa yanayoonyesha unyanyasaji wa watoto kingono (CSAM) ili kuzisaidia katika juhudi za kukabiliana na unyanyasaji huo kwenye mitandao yake. Kampuni kubwa, ikiwemo Google, zimejijumuisha kwenye orodha hii na zinachukua hatua muhimu ili kuondoa Maudhui yanayoonyesha unyanyasaji wa watoto kingono (CSAM) kwenye mifumo yao. Orodha hii pia huwezesha mashirika mengineyo yasiyo ya serikali (NGO) ambayo hutumikia watoto kutoa viwakilishi vifupi kwenye sekta ya teknolojia kupitia mfumo wa kiwakilishi kifupi wa Kituo cha Kitaifa cha Watoto Waliopotea na Wanaonyanyaswa (NCMEC), ili kujaribu kupunguza hitaji la kila kampuni ya teknolojia kwenda yenyewe kwenye kila shirika lisilo la serikali (NGO).
Pia, tunatoa mfumo wa Makampuni wa Kushiriki Kiwakilishi Kifupi, ambao huwezesha makampuni yaliochaguliwa kushiriki miongoni mwao viwakilishi vyake vifupi vya Maudhui yanayoonyesha unyanyasaji wa watoto kingono (CSAM). Tunahakikisha kuwa kampuni yoyote ambayo iko tayari na ina uwezo wa kugundua maudhui haya inapata zana zote zinazohitajika kufanya hivyo na kwamba makampuni yanaweza kushiriki viwakilishi vyake vifupi vya Maudhui yanayoonyesha unyanyasaji wa watoto kingono (CSAM) miongoni mwao. Google ni mchangiaji mkubwa wa mfumo huu ikiwa na takriban asilimia 74 ya jumla ya idadi ya viwakilishi vifupi kwenye orodha hiyo.
Ni wazi kwamba kwa kuzingatia idadi ya ripoti tunazopokea sasa, tunaona picha nyingi zinazofanana zikiripotiwa mara nyingi. Jambo hili linaeleweka kwani makampuni yanatumia viwakilishi vifupi kutambua maudhui yanayojulikana, lakini kadiri maudhui yanavyoongezeka, ni muhimu zaidi kwa Kituo cha Kitaifa cha Watoto Waliopotea na Wanaonyanyaswa (NCMEC) kuweza kubainisha maudhui mapya yaliyotayarishwa na kushirikiwa mtandaoni.
API ya Google ya Ulinganishaji Kiwakilishi imesaidia Kituo cha Kitaifa cha Watoto Waliopotea na Wanaonyanyaswa (NCMEC) kutoa kipaumbele kwa ripoti za mfumo wa CyberTipline. Je, unaweza kutueleza zaidi jinsi mradi huu ulivyoanza?
Mafanikio ya mpango wa kushiriki kiwakilishi yametupatia changamoto mpya: kiwango kikubwa cha ripoti za mtandaoni kimeleta changamoto kubwa zaidi. Shirika lisilo la faida la Kituo cha Kitaifa cha Watoto Waliopotea na Wanaonyanyaswa (NCMEC) halina uwezo wa kiteknolojia wa kushughulikia ripoti za mtandaoni za kiwango hiki. Ndio maana tunashukuru na kufurahi kwa ufadhili wa Google wa kuunda API ya Ulinganishaji Kiwakilishi.
Mwaka 2020 tulipokea ripoti milioni 21 za mfumo wa CyberTipline, lakini katika kila ripoti kunaweza kuwa na picha na video nyingi. Ripoti hizo milioni 21 zilijumuisha takriban picha na video milioni 70 za unyanyasaji wa watoto kingono. Ni dhahiri katika kiwango hicho kuna picha na video zinazofanana, na ingawa ni rahisi kwa Kituo cha Kitaifa cha Watoto Waliopotea na Wanaonyanyaswa (NCMEC) kutambua picha na video zinazofanana, tungeshindwa kutambua maudhui yanayofanana kwa upana na katika muda halisi ili kubainisha na kutoa kipaumbele kwa picha ambazo hazijawahi kuonekana awali. Jambo hilo ni muhimu zaidi tunapojaribu kutambua watoto wanaonyanyaswa kingono.
API ya Ulinganishaji Kiwakilishi imeleta manufaa gani kwa Kituo cha Kitaifa cha Watoto Waliopotea na Wanaonyanyaswa (NCMEC)?
Tuna jukumu la muhimu sana, ambalo ni kuchukua taarifa hizi muhimu na kuzituma haraka iwezekanavyo kwa mamlaka zinazotekeleza sheria. Mojawapo ya faida za zana hii ni kuwa inatupatia njia mpya ya kuongeza thamani kubwa kwa ripoti za mfumo wa CyberTipline.
Tumeandaa mpango mkakati ambapo tunapitia kila picha na video inayoonyesha unyanyasaji wa watoto kingono na kuipatia jina. Kwa mfano, ‘Haya ni Maudhui yanayoonyesha unyanyasaji wa watoto kingono (CSAM)’, ‘Haya si Maudhui yanayoonyesha unyanyasaji wa watoto kingono (CSAM)’, au ‘Ni vigumu kutambua umri wa mtoto au mtu husika.' Lakini, kama unavyoelewa, kuwa na faili milioni 70 kwa mwaka uliopita pekee ni ngumu kuzipatia majina zote. API hii inatuwezesha kufanya ulinganishaji. Tunapoweka alama kwenye faili moja API inatuwezesha kutambua faili zote pepe zinazofanana, kisha tutaziweka lebo ipasavyo katika muda halisi. Kutokana na hali hiyo, tumeweza kuwekea alama picha zaidi ya milioni 26.
Hatua hii hutusaidia kuongeza thamani katika ripoti tunazotuma kwa ajili ya utekelezaji wa sheria ili mamlaka ziweke kipaumbele ni ripoti gani watakazokagua kwanza. Pia inatusaidia kutambua ni picha gani ambazo hazijawahi kuonekana hapo awali. Picha hizo mara nyingi humwonyesha mtoto anayenyanyaswa kingono kutoka mahali fulani duniani. Tunafanya kila tunaloweza kwa namna yoyote kwa ajili ya kumsaidia mtoto anayehitaji kuokolewa. Zana ya Google imetuwezesha kuzingatia picha hizo za watoto wanaohitaji msaada wa haraka.
Je, teknolojia hiyo imeathiri kwa kiasi gani ustawi wa wakaguzi wa Kituo cha Kitaifa cha Watoto Waliopotea na Wanaonyanyaswa (NCMEC) wanaochakata ripoti za Kidokezo cha Mtandao na kuchanganua Maudhui yanayoonyesha unyanyasaji wa watoto kingono (CSAM)?
Zana hii ya utambuzi wa Maudhui yanayoonyesha unyanyasaji wa watoto kingono (CSAM) imepunguza hitaji la wafanyakazi wetu kupitia picha zinazofanana mara kadhaa. Kuna picha za watoto wakinyanyaswa kingono ambapo watoto hao huenda ni watu wazima sasa. Picha hizi daima zipo mtandaoni na mara kwa mara zinachangia uonevu unaoendelea wa waathirika hao. Hivyo, kuweza kuziwekea alama picha hizo huwawezesha kuwazingatia watoto hao wanaoonyeshwa kwenye unyanyasaji wa kingono wa hivi karibuni na wakati huo huo kuondoa picha hizo zinazokiuka sheria.
Ndio maana wafanyakazi wetu wapo hapa; wanataka kuwasaidia watoto hao. Haya yalikuwa maboresho mapya kabisa katika ufanisi wa wafanyakazi wetu ili waweze kufanya kazi kwa ubora na kuepuka kupitia maudhui yale yale, mara kadhaa.
Kazi hii inasaidiaje kampuni za teknolojia kwa ujumla kupambana na aina hii ya maudhui mtandaoni?
Tunafahamu kwamba Google hutoa teknolojia ya kutambua Maudhui yanayoonyesha unyanyasaji wa watoto kingono (CSAM) ili kusaidia kampuni kuunga mkono mapambano ya kimataifa dhidi ya maudhui hayo na API ya Kulinganisha Kiwakilishi ina manufaa kwa kampuni nyingi, zaidi ya Kituo cha Kitaifa cha Watoto Waliopotea na Wanaonyanyaswa (NCMEC). Kampuni zote za teknolojia zinafurahia faida ya mchakato ulioboreshwa zaidi na wenye ufanisi katika Kituo cha Kitaifa cha Watoto Waliopotea na Wanaonyanyaswa (NCMEC). Ripoti za mfumo wa CyberTipline zinashughulikiwa na kuchakatwa kwa wakati unaofaa na kwa thamani zaidi ikilinganishwa na kama hatungekuwa na zana hii.
Kituo cha Kitaifa cha Watoto Waliopotea na Wanaonyanyaswa (NCMEC) ni rasilimali kuu kwa kampuni za teknolojia, utekelezaji wa sheria, waathirika wa unyanyasaji na familia zao. Tuna uwezo wa kipekee sana unaotusaidia katika kuangalia matatizo na kuyatafutia suluhisho. Kwa sababu ya mfumo wa CyberTipline, tunatambua Maudhui mapya na yaliyokuwepo yanayosambazwa mtandaoni, yanayoonyesha unyanyasaji wa watoto kingono (CSAM). Ripoti hizi zote zinapatikana kwa ajili ya utekelezaji wa sheria. Kamwe hatufai kusahau kuwa, mwishowe, tuna watoto halisi waliodhulumiwa na kunyanyaswa kingono.
Tunafahamu zaidi ya watoto 20,000 waliotambuliwa ambao wamenyanyaswa kingono na unyanyasaji huo kunaswa kwenye video au picha. Waathirika hawa, baadhi bado ni watoto na wengine ni watu wazima sasa, wanafahamu kuhusu uonevu unaoendelea kuwahusu. Ndio maana ni muhimu sana kwetu kuchukua hatua tunayoweza ili kukabiliana na kupunguza kusambazwa kwa picha hizi.
Jambo ambalo huenda si dhahiri kwa umma ni kwamba kuna uwezekano wa kupuuza Maudhui yanayojulikana yanayoonyesha unyanyasaji wa watoto kingono (CSAM), kwa sababu picha hizo zinaweza kuchukuliwa kuwa "za zamani" au "zinazosambazwa tena". Tunafanya juhudi kila mara kuwakumbusha watu kuwa hawa ni watoto halisi na kwamba zaidi ya watu 20,000 wanajaribu kurejesha hali ya kawaida ya maisha yao. Wanapata faraja kufahamu kwamba kampuni kama vile Google zinafanya juhudi kuondoa picha zinazoonyesha matukio mabaya zaidi ya maisha yao.
Iwapo utaona picha zinazoonyesha unyanyasaji wa watoto kingono au maudhui mengineyo mtandaoni, unaweza kuripoti katika Kituo cha Kitaifa cha Watoto Waliopotea na Wanaonyanyaswa (NCMEC), au kwenye mamlaka husika duniani kote.
Google imejitolea kukabiliana na unyanyasaji wa watoto kingono mtandaoni pamoja na aina nyingine ya unyanyasaji wa watoto na kuzuia huduma zetu kutumika katika kusambaza maudhui yanayoonyesha unyanyasaji wa watoto kingono (CSAM). Unaweza kupata maelezo zaidi kuhusu suala hili kwenye tovuti yetu ya Kuwalinda watoto.