Kukagua shughuli za chinichini

Onyesho la nyuma ya pazia kuhusu jinsi Google inavyoimarisha zaidi usalama wa mtandaoni

Muundombinu

Google huendesha mojawapo ya miundombinu mikubwa na salama zaidi ya wingu ulimwenguni. Vituo vyake vya data vinapatikana duniani kote na vimeunganishwa na kebo za kioptiki za faiba za chini ya maji. Mfumo wote hufuatiliwa kwa makini kila wakati.

Google Play Protect

Kila siku, Play Protect hukagua karibu programu bilioni 50 za Android ili kubaini virusi na programu hasidi. Jaribio la kwanza hutokea wakati mtoa huduma anajaribu kupakia programu kwenye Duka la Google Play. Google Play Protect hutumika pia wakati watumiaji wanataka kupakua programu au kuitumia kwenye vifaa vyao. Huduma hii inapotambua programu inayoweza kuwa hasidi, Google humwonya mtumiaji au kuondoa programu kiotomatiki. Kwa maelezo zaidi, tembelea android.com.

Usimbaji fiche

Google hutumia teknolojia mbalimbali za usimbaji fiche kama vile HTTPS na TLS ili kulinda barua pepe zinazotumwa kupitia Gmail na picha ambazo watumiaji huhifadhi kwenye wingu. Mtambo wa kutafuta wa Google hutumia pia itifaki ya HTTPS kama teknolojia ya kawaida.

Kukagua maombi ya data

Google haitoi idhini ya moja kwa moja ya kufikia data ya watumiaji kwa mashirika ya kijasusi au mashirika mengine ya serikali. Hali hiyo pia inatumika Marekani na Ujerumani jinsi ilivyo katika kila nchi duniani. Ikiwa mamlaka fulani itaomba uwezo wa kufikia data ya mtumiaji, Google itachunguza ombi hilo na haitatoa uwezo wa ufikiaji bila sababu nzuri. Google imechapisha ripoti za uwazi kwa miaka mingi, ambazo ni pamoja na maombi ya data. Ili usome ripoti hizi, tembelea transparencyreport.google.com.

Kuvinjari salama

Teknolojia ya Kipengele cha Kuvinjari Salama na Google hulinda watumiaji dhidi ya tovuti hatari na watendaji hasidi. Katika kiini chake, kuna hifadhidata iliyo na anwani za tovuti zinazoshukiwa. Ikiwa mtumiaji atajaribu kutembelea mojawapo ya tovuti hizi, atapokea onyo. Google hutumia pia uhalisi pepe ili kukabiliana na mbinu mpya zinazobuniwa za wizi wa data binafsi. Ili upate maelezo zaidi, tembelea safebrowsing.google.com.

Kuzuia mapengo kwenye usalama

Kila mwaka, Google huwekeza mamilioni ya dola kwenye miradi ya utafiti – na kwenye “zawadi kwa watambuzi wa hitilafu katika programu.” Zawadi hizi ni za wataalamu wa TEHAMA wanaosaidi kampuni kupata mapengo yaliyojificha ya usalama. Mtaalamu mmoja kama huyo ni Ezequiel Pereira mwenye umri wa miaka 18 kutoka Urugwai, ambaye amesaida Google kutambua mapengo kadhaa kama hayo. Mwaka uliopita, alipokea zawadi ya dola 36,337 kwa sababu ya ugunduzi muhimu.

Project Zero

Timu mahiri ya usalama wa Google hujitahidi kuziba mapengo ya usalama kabla ya wadukuzi na wezi wa data kuyapata. Wataalamu huiita mianya hii “Athari za zero-day (athari zisizojulikana kwa wale ambao wangependa kuziepuka),” ndio maana timu hiyo inajulikana kama Project Zero. Timu haizingatii tu huduma za Google; hutafuta pia udhaifu kwenye huduma za washindani, ili iweze kuwaarifu kuhusu suala hili na kusaidia kuwalinda watumiaji wao pia. Kwa maelezo zaidi kuhusu kazi ya timu ya Project Zero, tembelea googleprojectzero.blogspot.com.

Usaidizi wa ziada kwa watoa huduma wengine wa TEHAMA

Google huendelea kufanya teknolojia zake za usalama zipatikane kwa kampuni zingine bila malipo kwa lengo la kudumisha usalama wa mtandaoni, hata nje ya huduma za Google. Kwa mfano, wasanidi programu kwenye kampuni nyingine wanaweza kutumia teknolojia ya Cloud Security Scanner ili kutafuta athari za usalama. Teknolojia ya Kipengele cha Kuvinjari Salama na Google hutumiwa na kivinjari cha Safari cha Apple na Mozilla Firefox.

Ulinzi dhidi ya barua taka kwa usaidizi wa uhalisia pepe

Google hutumia teknolojia ya mashine kujifunza ili kulinda watumiaji wa Gmail dhidi ya barua taka. Mitandao ya algoriti za utambuzi wa uhusiano wa msingi katika kikundi cha data huchanganua mabilioni ya barua pepe ambazo hazihitajiki au ambazo hazitakikani na kutambua ruwaza ambazo huiruhusu kutambua barua taka. Mbinu imethibitishwa kuwa fanisi. Sasa, barua pepe taka zisizozidi moja kati ya elfu hufaulu kupatikana kwenye vikasha vya mtumiaji – na idadi hiyo inapungua kila siku!

Pata maelezo zaidi katika:

safety.google

Michoro: Robert Samuel Hanson

Fahamu jinsi ambavyo Google husaidia kulinda usalama wa kila mtu mtandaoni.