Kila bidhaa ya Google
imebuniwa kwa usalama.
Kila siku, mabilioni ya watu hutumia Google kupata maelezo ya kuaminika, kufika wanakoenda, kuwasiliana na wapendwa wao na zaidi. Unapotumia bidhaa na huduma zetu, ni wajibu wetu kuhifadhi taarifa zako binafsi kwa usalama na faragha.
Kwa njia salama.
-
Matokeo salama na yenye ubora wa juu
Tunajitahidi kuhakikisha kuwa unaona matokeo ya utafutaji yaliyo muhimu na yenye ubora wa juu, wala si taka ya wavuti, kama vile tovuti ambazo hazitoi maudhui yenye ubora wa juu au hutumia mbinu ambazo zinaweza kuwa hatari kwa watumiaji. Tunaendelea kuboresha teknolojia yetu ya kukabili taka na kufanya kazi na wasio kwenye Google ili kudumisha wavuti ulio salama na wenye ubora wa juu.
-
Utafutaji wako umelindwa
Utafutaji wote kwenye google.com na kwenye programu ya Google husimbwa kwa njia fiche kwa chaguomsingi ili unachotafuta kilindwe.
-
Vidhibiti vya faragha ambavyo ni rahisi kutumia
Tunaimarisha usalama wa Historia ya mambo uliyotafuta na kukurahisishia mchakato wa kukagua na kuifuta kwenye akaunti yako kwa kutumia vidhibiti vya faragha.
-
Vithibiti kwa usalama wa maudhui
Huduma ya Tafuta imebuniwa kukusaidia kupata unachotafuta. Unaweza kuweka safu ya ulinzi kwa kujijumuisha kwenye mpango wa Utafutaji Salama, unaoweza kusaidia kuchuja matokeo ya maudhui yaliyo na ngono dhahiri.
-
Tafuta katika Hali fiche ukitumia programu ya Google
Programu ya Google ya iOS ina Hali fiche. Kwa kawaida unaweza kuifikia kwa kubofya tu mara moja kwenye skrini ya kwanza.
taarifa zako za faragha kwa njia salama.
-
Ulinzi thabiti dhidi ya wizi wa data binafsi
Mashambulizi mengi ya programu hasidi na ya wizi wa data binafsi huanza kwa barua pepe. Gmail huzuia zaidi ya asilimia 99.9 ya barua taka, majaribio ya wizi wa data binafsi na programu hasidi zisikuathiri.
-
Usalama wa akaunti
Tunalinda akaunti yako dhidi ya shughuli za kuingia katika akaunti zinazotiliwa shaka na zile ambazo hazijaidhinishwa kwa kufuatilia viashiria kadhaa vya usalama. Pia tunatoa Mpango wa Ulinzi wa Hali ya Juu kwa akaunti zilizo katika hatari kubwa ya mashambulizi mahususi.
-
Usimbaji wa barua pepe
Kwenye mfumo wa Google, ujumbe husimbwa ukiwa umehifadhiwa na unapotumwa kati ya vituo vya data. Ujumbe unaotumwa kwa watoa huduma wengine husimbwa na mbinu ya Transport Layer Security panapowezekana au inapohitajika na mipangilio.
-
Ni salama kwa chaguomsingi
Ulinzi uliobuniwa ndani ya mfumo kama vile Kuvinjari Salama, utaratibu wa kuweka vikwazo na teknolojia nyingine bora zaidi za kukulinda dhidi ya tovuti hatari, programu hasidi na vitisho unapotumia Chrome.
-
Masasisho ya usalama ya kiotomatiki
Chrome inaweza kusasisha kiotomatiki kila baada ya wiki sita ili uwe na vipengele na marekebisho mapya ya usalama, huhitaji kuchukua hatua yoyote.
-
Manenosiri thabiti na ya kipekee
Ili kuimarisha usalama wa akaunti zako zote, Chrome inaweza kusaidia kutunga manenosiri thabiti na ya kipekee na kuyaweka kwenye vifaa vyako unapovinjari kwenye wavuti.
-
Hali Fiche
Hali Fiche katika Chrome hukupa chaguo la kuvinjari intaneti bila shughuli zako kuhifadhiwa kwenye kivinjari au kifaa chako.
dhibiti faragha yako.
-
Hali Fiche
Tumia Ramani katika Hali Fiche na shughuli zako hazitahifadhiwa kwenye kifaa chako. Washa Hali Fiche kwenye Ramani kwa urahisi kwa kugusa picha ya wasifu wako, na uizime wakati wowote ili upate hali ya utumiaji inayokufaa zaidi, yakiwemo mapendekezo ya mikahawa na vipengele vingine vinavyokufaa.
-
Vidhibiti vya faragha ambavyo ni rahisi kufikia
Kwa kutumia “Data yako kwenye Ramani,” unaweza kufikia Kumbukumbu ya Maeneo Yako na vidhibiti vingine vya faragha kwa urahisi ili uone na udhibiti data yako.
hali yako ya utumiaji wa YouTube.
-
Mipangilio ya Matangazo
Hatuuzi kamwe taarifa zako binafsi kwa mtu yeyote. Tunatoa pia mipangilio ya matangazo ili uweze kudhibiti vyema matangazo unayoona na kuzima mipangilio ya kuweka mapendeleo ya matangazo kwenye Mipangilio ya Matangazo.
-
Hali Fiche
Wakati Hali Fiche imewashwa kwenye YouTube, shughuli zako – kama vile video unazotazama – hazitahifadhiwa kwenye Akaunti yako ya Google wala kujumuishwa kwenye historia ya video ulizotazama.
-
Vidhibiti vya faragha ambavyo ni rahisi kutumia
Historia yako ya YouTube inaweza kuboresha hali yako ya utumiaji na kutoa mapendekezo ya maudhui. Amua muda ambao utahifadhi Historia yako ya YouTube au uizime kwa kwenda kwenye “Data Yako kwenye YouTube.”
la kuhifadhi kumbukumbu za maisha.
-
Kulinda taarifa yako
Tunalinda nakala za kumbukumbu unazohifadhi katika programu ya Picha kwenye Google kwa kutumia mojawapo ya miundombinu ya usalama ambayo ni thabiti zaidi ulimwenguni. Tunasimba pia kwa njia fiche taarifa yako inapotumika kati ya kifaa chako, huduma za Google na vituo vyetu vya data.
-
Kushughulikia data kwa kuwajibika
Programu ya Picha kwenye Google haiuzi picha, video au taarifa zako binafsi kwa mtu yeyote na hatutumii picha na video zako kwa matangazo. Vipengele kama vile kupanga picha kulingana na nyuso za waliomo hurahisisha mchakato wa kutafuta na kudhibiti picha zako. Hata hivyo, ni wewe tu unayeweza kuona picha zilizopangwa kulingana na nyuso za waliomo na hatubuni teknolojia yenye madhumuni ya jumla ya utambuzi wa sura kwa lengo la kibiashara.
-
Kukupa uwezo wa kudhibiti
Tulibuni zana za kutumiwa kwa urahisi zinazokusaidia kudhibiti hali yako ya utumiaji wa programu ya Picha kwenye Google. Unaweza kuhifadhi nakala za picha unazochagua kwenye wingu, kushiriki picha zako kwa njia salama, kuzima kipengele cha picha zilizopangwa katika makundi kulingana na nyuso za waliomo na lebo ili uzifute kwenye akaunti yako na kufanya mabadiliko kwenye maelezo ya mahali.
uliobuniwa kukulinda.
-
Google Play Protect
Google Play Protect huchanganua kiotomatiki programu zako ili kuhakikisha kuwa ni salama. Ukipata programu mbaya, tutakuarifu haraka na kukuagiza kuhusu jinsi ya kuiondoa kwenye kifaa chako.
-
Idhini za programu
Programu unazopakua hutumia data kwenye kifaa chako kufanya utendaji wake uwe muhimu zaidi. Idhini za programu zinakupa udhibiti iwapo na wakati programu inaweza kufikia aina tofauti za data kwenye kifaa chako, kama vile anwani, picha na data ya mahali.
-
Ulinzi dhidi ya wizi wa data binafsi
Wizi wa data binafsi hutokea wakati mtu anajaribu kukulaghai umpe taarifa yako ya faragha. Android hukupa tahadhari kuhusu wanaotuma taka na kipengele cha Kuchuja Simu hukuruhusu uulize anayekupigia kabla ya kupokea simu.
-
Vipengele vya usalama ambavyo huwa vimewashwa kwa chaguomsingi
Ili kulinda mikutano kwa usalama, Google Meet ina vipengele vya kuzuia matumizi mabaya na vidhibiti salama vya mikutano ambavyo huwa vimewashwa kwa chaguomsingi na huruhusu chaguo nyingi za uthibitishaji wa hatua mbili, zikiwemo funguo za usalama.
-
Mipangilio ya usimbaji fiche wakati mikutano inaendelea huwa imewashwa kwa chaguomsingi
Mikutano yote ya video husimbwa kwa njia fiche inapoendelea. Meet inatii viwango vya usalama vya IETF vya Datagram Transport Layer Security (DTLS).
-
Utumiaji rahisi na salama
Hatuhitaji programu jalizi ili kutumia Meet kwenye wavuti. Hufanya kazi kikamilifu kwenye Chrome na vivinjari vingine, kwa hivyo haishambuliwi kwa urahisi. Kwenye kifaa cha mkononi, unaweza kusakinisha programu ya Google Meet.
kuimarisha usalama wako mtandaoni.
-
Usalama na faraghaPata maelezo kuhusu jinsi Google hulinda taarifa zako za faragha na kukupatia uwezo wa kuzidhibiti.
-
Usalama wa maudhuiPata maelezo kuhusu jinsi tunavyowasilisha maelezo ya kuaminika ili kuhakikisha intaneti ni salama kwa wote.
-
Usalama wa familiaPata maelezo kuhusu jinsi Google inavyokusaidia udhibiti maudhui yanayofaa familia yako mtandaoni.
-
Usalama wa mtandaoniPata maelezo kuhusu jinsi tunavyohakikisha usalama wa watu wengi zaidi mtandaoni kuliko mtu mwingine yeyote duniani.