Jinsi ya kuwa na data yako popote ulipo
Ungependa kupakua data binafsi kwenye kompyuta yako au kuihamishia kwa mtoa huduma mwingine? Yote yanawezekana kwa kutumia Google Takeout, jinsi inavyofafanuliwa na Stephan Micklitz na Greg Fair kutoka Google
Bw. Micklitz, Bw. Fair, unasimamia programu ya Google Takeout. Ina umuhimu gani hasa?
Stephan Micklitz, Mkurugenzi wa Uhandisi katika timu ya Faragha na Usalama ya Google: Google Takeout inakuwezesha, kwa mfano, upakue picha, anwani za mawasiliano, barua pepe, data ya kalenda au faili za muziki zilizohifadhiwa kwenye Hifadhi ya Google katika kompyuta yako au kuzihamishia kwa mtoa huduma mwingine.
Greg Fair, Msimamizi wa Bidhaa wa Google Takeout: Mimi na mke wangu tuna watoto wawili na kama wazazi wengine wengi, tuna picha zao nyingi sana – picha zinazoweza kuchukua nafasi ya hifadhi ya Gigabaiti 600, kwa hakika. Diski kuu yetu iliyo na picha hizi zote ilipoacha kufanya kazi, nilifurahi sana kwa sababu nilikuwa nimezihifadhi pia picha zote kwenye programu ya Picha kwenye Google. Kisha niliweza kutumia programu ya Google Takeout kupakua tu picha kwa urahisi kwenye diski kuu mpya.
Watu hutumiaje programu ya Takeout?
Fair: Zaidi ni katika kuhifadhi nakala ya data yote wanayoweka kwenye Hifadhi ya Google.
Micklitz: Jambo ambalo halina mantiki kwa kiasi fulani, kwa sababu data ni salama zaidi kwenye Hifadhi ya Google kuliko jinsi ilivyo katika vifaa vyetu vingi vya kuhifadhia nyumbani.
Fair: Ukiwa nyumbani, paka anaweza kuchafua diski kuu au watoto wanaweza kuivunja au ajali ya moto inaweza kutokea nyumbani. Katika Google, kila faili huhifadhiwa mara kadhaa kwenye seva tofauti. Ni njia salama zaidi ya kuhifadhi faili.
Na bado pia unahifadhi nakala ya data yako kwenye diski kuu, Bw. Fair!
Fair: Hiyo ni kwa sababu mke wangu hutumia programu za kuhariri picha ambapo haiwezekani kuhifadhi picha kwenye wingu.
"Kwenye Google, kila faili huhifadhiwa mara kadhaa kwenye seva tofauti. Ni njia salama zaidi ya kuhifadhi faili."
Greg Fair
Vyema.
Micklitz: Lakini mimi kwa mfano, situmii programu kama hiyo, lakini bado ninahifadhi nakala za picha zangu zote kwenye diski kuu. Ni data yangu, kwa hivyo ningependa kuwa na nakala halisi.
Kwa nini uwe na matendo “yasiyo na mantiki”?
Micklitz: Tunathamini sana picha zetu. Zinahusishwa na kumbukumbu nyingi sana. Kama mtumiaji, singependa kuwa katika nafasi ambapo ninategemea kampuni moja kuhifadhi picha zangu kwa usalama – hata kama ni kampuni ninayoifanyia kazi. Ndiyo maana huduma za uwezo wa kubeba data kama vile Google Takeout ni muhimu sana, kwa sababu zinawapa watumiaji uwezo wa kupata tena data yao wakati wowote – hata kama imehifadhiwa kwenye wingu.
Mada kuhusu uwezo wa kubeba data imekuwa muhimu kwenye Google tangu lini?
Fair: Kwa zaidi ya mwongo mmoja. Tulianza kwa kubuni huduma mahususi za uwezo wa kubeba data. Kisha, mwaka wa 2011, Google ilizindua huduma yake kuu: Takeout. Tumejumuisha huduma nyingi zaidi za Google tangu wakati huo na kwa sasa, Takeout inatumika katika zaidi ya huduma 40.
Ingawa watumiaji wengi hupakua data yao kwenye kompyuta zao, si rahisi waihamishie kwenye huduma zingine. Kwa nini kuna tofauti hii?
Fair: Siku hizi, bila shaka watumiaji wanaweza kuhamisha data yao kutoka Google hadi Dropbox, Box au Microsoft Office 365 – na kutoka huduma hizo hadi kwenye Google. Washindani wetu wengi bado hawatoi huduma hii. Ili kujaribu kubadilisha hali hiyo, tulianzisha Mradi wa Uhamishaji wa Data mwaka wa 2017 na kutangaza rasmi mradi huo mnamo Julai 2018. Huu ni mradi wa programu huria ambao unazipatia kampuni msimbo usiolipishwa kwa ajili ya vipengele vyenye uwezo wa kubeba data, hali inayowezesha uhamishaji rahisi wa data kutoka huduma moja hadi nyingine.
Micklitz: Ikiwa kampuni mpya itabuni huduma mpya bora zaidi. Itakuwa ghali sana kwa kampuni ndogo kubuni huduma yake binafsi yenye uwezo wa kubeba data. Badala yake, inaweza kutumia Mradi wa Kuhamisha Data na kuhamishia misimbo inayolingana kwenye programu yake binafsi.
Lakini ni kwa nini ungependa nibadilishe mtoa huduma?
Fair: Tungependa utumie huduma za Google kwa sababu ni bora zaidi, si kwa sababu unafikiri kuwa huwezi kutumia data yako mahali pengine.
Sheria ya Jumla ya Ulinzi wa Data, iliyoanza kutekelezwa mnamo Mei 2018, ina sheria kuhusu uwezo wa kubeba data. Je, ulihitaji kuweka mapendeleo ya zana yako ya kupakua data ili kutimiza masharti haya?
Fair: Tuliposoma sheria kwa mara ya kwanza mwaka wa 2016, tulitambua kuwa tulikuwa tunafanya kazi nzuri kuhusiana na suala la uwezo wa kubeba data. Hata kabla ya wakati huo, tulikuwa tumeishughulikia kwa kina mada hii kwa muda fulani.
Micklitz: Tunafikiri kuwa hatimaye mada hii inaangaziwa kikamilifu. Kwa sasa, bado suala la uwezo wa kubeba data ni fursa ambayo haijagunduliwa na watumiaji wengi. Lakini tunaamini kuwa hali hii itabadilika baada ya miaka michache.
"Watoto wangu wanapaswa kuwa na picha kuanzia walipokuwa watoto wachanga, jinsi nilivyo nazo."
Stephan Micklitz
Kwa nini?
Micklitz: Watu wameanza kuhifadhi data yao kwenye wingu hivi majuzi tu. Kwa mfano, tuchukulie kuwa kampuni hiyo inafilisika na data yako imehifadhiwa kwenye seva za kampuni hiyo. Ungependa kujua ikiwa unaweza kurejesha data hii. Ni suala linalohusu pia mada ya uwezo wa kudumu kwa data. Watoto wangu wanapaswa kuwa na picha za kuanzia walipokuwa wachanga, jinsi ninavyotazama picha za zamani za wazazi wangu.
Je, ungependa picha za dijitali zidumu kwa muda mrefu kama picha za analogi?
Micklitz: Ndiyo. Hiki pia ni kipengele cha ulinzi wa data katika taswira pana – kwa kuwa bado nitaweza kutumia data ninayohifadhi leo kwa kipindi cha miaka 50 ijayo.
Picha: Conny Mirbach
Uboreshaji wa usalama mtandaoni
Pata maelezo kuhusu jinsi tunavyohakikisha usalama wa watu wengi zaidi mtandaoni kuliko shirika lolote lingine duniani.
Pata maelezo zaidi