Kulinda faragha yako
huanza na miundombinu ya usalama
ambayo ni thabiti zaidi ulimwenguni.
Bidhaa zote za Google zinalindwa kila wakati na mojawapo ya miundombinu ya usalama ambayo ni thabiti zaidi ulimwenguni. Usalama huu uliojumuishwa hutambua na kuzuia kiotomatiki hatari za mtandaoni, ili upate uhakika kuwa taarifa yako ya faragha iko salama.
kupitia usalama
unaosasishwa kila mara.
Usimbaji fiche
Usimbaji fiche hudumisha faragha na usalama wa data inapotumwa
Usimbaji fiche huboresha kiwango cha usalama na faragha kwenye huduma zetu. Unapotuma barua pepe, kushiriki video, kutembelea tovuti au kuhifadhi picha zako, data unayotengeneza hupitia kwenye kifaa chako, huduma za Google na vituo vyetu vya data. Tunalinda data hii kwa kutumia vidhibiti vingi vya usalama, ikiwa ni pamoja na teknolojia maarufu ya usimbaji fiche kama vile HTTPS na TLS.
Arifa za Usalama
Arifa hima za usalama husaidia kulinda maelezo yako ya faragha
Tutakuarifu kwa hima tukitambua kitu ambacho tunaona kuwa unapaswa kujua kuhusu, kama vile hatua ya kutiliwa shaka ya kuingia katika akaunti au tovuti, faili au programu hasidi na tutakupa mwongozo wa kukusaidia kuimarisha usalama wako. Kwa mfano, kwenye Gmail, tutakuonya kabla ya kupakua kiambatisho ambacho kinaweza kuhatarisha usalama wako au iwapo mtu ataingia katika akaunti yako akitumia kifaa ambacho hakihusishwi nawe. Tukitambua shughuli zinazotiliwa shaka katika akaunti yako, tutatuma arifa kwenye kikasha chako au kwenye simu yako ili uweze kulinda akaunti yako haraka zaidi.
Kuzuia matangazo mabaya
Kuzuia matangazo hasidi na yanayopotosha kabla yakufikie
Usalama na hali yako ya utumiaji mtandaoni inaweza kuathiriwa na matangazo yaliyo na programu hasidi, yanayofunika maudhui unayojaribu kuona, yanayotangaza bidhaa bandia, au kukiuka vinginevyo sera zetu za matangazo. Tunachunguza tatizo hili kwa makini. Kila mwaka, tunazuia mamilioni ya matangazo yasiyofaa – kwa wastani takribani matangazo 100 kwa kila sekunde – kupitia usaidizi wa wakaguzi wa moja kwa moja na programu za hali ya juu. Tunakupa pia zana za kuripoti matangazo yanayokera na kudhibiti aina za matangazo unayoona. Na tunachapisha kila wakati maarifa na mbinu bora zaidi za kuimarisha usalama wa intaneti kwa manufaa ya kila mtumiaji.
Usalama wa Wingu
Miundombinu yetu ya wingu hulinda data wakati wote
Kuanzia vituo maalum vya data hadi kebo zetu baharini ambazo husafirisha data kati ya mabara, Google hutumia mojawapo ya miundombinu ya wingu ambayo ni thabiti na salama zaidi ulimwenguni. Hufuatiliwa kila wakati ili kulinda data yako na kuifanya ipatikane. Na kukitokea tukio la kukatiza, huduma za mfumo zinaweza kuhamishwa kiotomatiki na papo hapo kutoka eneo moja hadi lingine ili ziweze kuendelea bila kukatizwa.
ZANA ZA UTHIBITISHAJI
Kuingia katika akaunti zako zote za mtandaoni kwa njia salama
Akaunti za mtandaoni hukupa uwezo wa kufikia huduma muhimu zinazokufaa, lakini hatua ya kuingia katika akaunti hizo inaweza kusababisha hatari kubwa zaidi za usalama siku hizi. Kila siku, mamilioni ya manenosiri hufichuliwa katika matukio ya ufichuzi haramu wa data, hali ambayo inaweza kuhatarisha taarifa zako za faragha.
Zana zetu za uthibitishaji zilizojumuishwa zimebuniwa ili kukusaidia uingie katika akaunti kwenye huduma na programu uzipendazo kwa haraka na kwa njia salama.
unazotumia kila siku.
-
Gmail hukulinda dhidi ya
barua pepe zinazotiliwa shaka na kukuonya dhidi ya hatariMashambulizi mengi ya programu hasidi na ya wizi wa data binafsi huanza kwa barua pepe. Gmail hukulinda vizuri dhidi ya barua taka, wizi wa data binafsi na programu hasidi ikilinganishwa na huduma nyingine yoyote ya barua pepe. Kwa kutumia mashine ya kujifunza na utashi wa kompyuta, Gmail hukagua miundo inayotokana na mamilioni ya ujumbe ili kutambua sifa za barua pepe ambazo watumiaji wameripoti kuwa taka, kisha hutumia sifa hizo kuzuia asilimia 99.9 ya barua pepe hizo hatari au zinazotiliwa shaka kabla zifikie kikasha chako.
-
Masasisho ya kiotomatiki ya Chrome hukulinda
dhidi ya programu hasidi na tovuti zinazopotoshaTeknolojia za usalama hubadilika kila wakati. Kwa hivyo, Chrome hukagua mara kwa mara ili kuhakikisha kwamba toleo la kivinjari unachotumia ni jipya zaidi. Hii inajumuisha marekebisho mapya ya usalama na ulinzi dhidi ya programu hasidi na tovuti zinazopotosha. Na Chrome inaweza kusasisha kiotomatiki, kwa hivyo unalindwa kwa urahisi kupitia teknolojia mpya ya usalama.
-
Kulinda usalama wa kifaa cha Android, programu
na data yako kwa kutumia Google Play ProtectGoogle Play Protect imejumuishwa kwenye kifaa chako cha Android na huendelea kufanya kazi unapotumia kifaa chako ili kudumisha usalama wa kifaa, data na programu zako. Kila siku, sisi huchanganua kiotomatiki programu kwenye simu za Android na kujitahidi ili kuzuia programu hatari zisizifikie, hali inayofanya Google Play Protect iwe huduma inayotumiwa zaidi duniani kwa ulinzi dhidi ya hatari kwenye vifaa vya mkononi.
kuimarisha usalama wako mtandaoni.
-
Vidhibiti vya faraghaChagua mipangilio ya faragha inayokufaa.
-
Kanuni za dataPata maelezo zaidi kuhusu jinsi tunavyoheshimu faragha yako kwa kutumia kanuni za data.
-
Vidokezo vya usalamaGundua vidokezo vya haraka na desturi bora za kuwa salama mtandaoni.
-
Matangazo na dataPata maelezo zaidi kuhusu matangazo unayoonyeshwa kwenye mifumo yetu.