Zana za faragha ambazo
zinakupa uwezo wa kudhibiti.

Tunajua kuwa suala la faragha halishughulikiwi kwa njia moja pekee. Ndiyo maana tunaunda vidhibiti ambavyo ni rahisi kutumia ili uweze kuchagua mipangilio ya faragha ambayo inakufaa.

Dhibiti data inayohifadhiwa
kwenye Akaunti yako ya Google

Vidhibiti vya Shughuli

Dhibiti data inayohifadhiwa

Kwa kutumia Vidhibiti vya Shughuli, unaweza kubainisha aina za shughuli zitakazohusishwa na akaunti yako ili kuweka mapendeleo ya hali yako ya utumiaji kwenye huduma zote za Google. Unaweza kusitisha aina mahususi za data zisihifadhiwe kwenye akaunti yako – kama vile shughuli zako za huduma ya Tafuta na Google na kuvinjari, Historia ya YouTube au Kumbukumbu ya Maeneo Yangu.

Nenda kwenye Vidhibiti vya Shughuli

Futa Kiotomatiki

Weka mipangilio ya kufuta kiotomatiki data yako

Ili kukupa uwezo zaidi wa kudhibiti, mipangilio ya kufuta kiotomatiki inakuwezesha uchague kipindi ambacho ungependa kuhifadhi data ya shughuli zako. Data ambayo muda wake wa kuhifadhiwa umepita kipindi ulichochagua itaendelea kufutwa kiotomatiki kwenye akaunti yako. Hatua hii inakurahisishia shughuli ya kuiweka na kuisahau, lakini unaweza kurudi na kusasisha mipangilio hii wakati wowote.

Futa kiotomatiki shughuli zako

Shughuli Zangu

Futa data kwenye akaunti yako wakati wowote

Sehemu ya Shughuli Zangu ni mahali ambapo unaweza kupata mambo yote ambayo umetafuta, kuangalia na kutazama kwa kutumia huduma zetu. Ili uweze kukumbuka mambo uliyotafuta awali mtandaoni kwa urahisi, tunakupa zana za kutafuta kulingana na mada, tarehe na bidhaa. Unaweza kufuta kabisa shughuli mahususi au hata mada zote ambazo huhitaji katika akaunti yako.

Tembelea ukurasa wa Shughuli Zangu
Chagua mipangilio ya
faragha
ambayo
inakufaa.

Ukaguzi wa Faragha

Fanya Ukaguzi wa Faragha

Kwa dakika chache tu, unaweza kuchagua aina za data ambazo ungependa zihifadhiwe kwenye Akaunti yako ya Google, kusasisha data unayoshiriki na marafiki au kuifanya ipatikane hadharani na kurekebisha aina za matangazo ambayo ungependa tukuonyeshe. Unaweza kubadilisha mipangilio hii mara kwa mara kadri upendavyo na hata uchague kutumiwa vikumbusho vya mara kwa mara.

Dhibiti faragha yako,
moja kwa moja kwenye programu zako
unazotumia kila siku.

Hali Fiche

Washa hali Fiche kwenye Chrome, Tafuta na Google, YouTube na Ramani

Tangu ilipozinduliwa kwa mara ya kwanza kwenye Chrome, sasa hali fiche inapatikana kwenye programu zetu nyingi maarufu zaidi. Kwenye YouTube, huduma ya Tafuta kwenye iOS na Ramani, gusa tu picha yako ya wasifu ili uiwashe au uizime kwa urahisi. Unapowasha Hali fiche kwenye Ramani na YouTube, shughuli zako kama vile maeneo unayotafuta au video unazotazama, hazitahifadhiwa kwenye Akaunti yako ya Google. Vidakuzi na historia ya kuvinjari kutoka kwenye kipindi chako fiche hufutwa kwenye Chrome pindi unapofunga madirisha yote Fiche.

Data Yako Katika

Dhibiti data yako moja kwa moja kwenye programu zako

Tumekurahisishia shughuli ya kufanya maamuzi kuhusu data yako moja kwa moja kwenye huduma za Google unazotumia kila siku. Kwa mfano, bila kuondoka kwenye huduma ya Tafuta, unaweza kukagua na kufuta shughuli zako za utafutaji za hivi majuzi, kufikia kwa haraka vidhibiti vya faragha vinavyohusiana kwenye Akaunti yako ya Google na kupata maelezo zaidi kuhusu jinsi huduma ya Tafuta hufanya kazi kwa kutumia data yako. Unaweza kufikia vidhibiti hivi kwenye huduma ya Tafuta na Google, Ramani na programu ya Mratibu wa Google.

Gundua njia zaidi tunazotumia
kulinda usalama wako mtandaoni.