Tunalinda taarifa zako binafsi
kwa njia salama na ya faragha.

Katika Google, tunaheshimu na kulinda faragha yako kwa kutumia mbinu bora zaidi za usalama, kanuni za data zenye uwajibikaji na zana za faragha ambazo ni rahisi kutumia, zinazokupa uwezo wa kudhibiti.

Kulinda faragha yako
huanza na mfumo thabiti zaidi
wa usalama ulimwenguni.

Faragha yako imelindwa kwenye bidhaa zote za Google kwa kutumia ulinzi uliojumuishwa kwenye mfumo uliobuniwa kuzuia hatari kiotomatiki kabla ya zifikie data yako.

Pata maelezo zaidi

Usimbaji fiche wa kina hulinda usalama wa data yako inapotumwa

Usimbaji fiche huboresha kiwango cha usalama na faragha kwenye huduma zetu. Unapotuma barua pepe, kushiriki video, kutembelea tovuti au kuhifadhi picha zako, data unayotengeneza hupitia kwenye kifaa chako, huduma za Google na vituo vyetu vya data. Tunalinda data hii kwa kutumia vidhibiti vingi vya usalama, ikiwa ni pamoja na teknolojia maarufu ya usimbaji fiche kama vile HTTPS na TLS.

Arifa za hima za usalama husaidia kulinda maelezo yako ya faragha

Tutakuarifu kwa hima tukitambua kitu ambacho tunaona kuwa unapaswa kukijua - kama vile hatua ya kutiliwa shaka ya kuingia katika akaunti au tovuti, faili au programu hasidi - na tutakupa mwongozo wa kukusaidia kuimarisha usalama wako. Tukitambua shughuli zinazotiliwa shaka katika akaunti yako, tutatuma arifa kwenye kikasha chako au kwenye simu yako ili uweze kulinda akaunti yako haraka zaidi.

Hatari hutambuliwa na kuzuiwa kiotomatiki

Kipengele cha Kuvinjari Salama hulinda vifaa bilioni 5 kila siku kikiwemo chako. Ili kufanya intaneti iwe salama kwa manufaa ya kila mtu, tuliruhusu kampuni nyingine zitumie teknolojia hii bila malipo katika vivinjari vyao, ikiwa ni pamoja na Apple Safari na Mozilla Firefox. Kwa hivyo unalindwa unapovinjari kwenye Google na bidhaa zingine.

Zana za faragha ambazo ni rahisi kutumia
zinazokupa uwezo wa kudhibiti.

Dhibiti data inayohifadhiwa kwenye Akaunti yako ya Google

Tunajua kuwa suala la faragha halishughulikiwi kwa njia moja pekee. Hiyo ndiyo maana tunakusaidia uchague mipangilio ya faragha ambayo inakufaa. Iwe unataka kuhifadhi, kufuta au kufuta kiotomatiki data yako, tunakupatia zana za kutekeleza shughuli hizo.

Faragha yako inalindwa na
kanuni za data zenye uwajibikaji.

Data huwa muhimu katika kuboresha bidhaa na huduma unazotumia kila siku. Tumejitolea kushughulikia data kwa kuwajibika na kulinda faragha yako kwa kutumia itifaki thabiti na teknolojia bunifu za faragha.

Gundua mbinu zaidi tunazotumia
kuimarisha usalama wako mtandaoni.