Mahali salama
pa kuweka kumbukumbu za maisha.
Programu ya Picha kwenye Google ni mahali ambako picha na video zako zote huhifadhiwa, kupangwa kiotomatiki na kutumiwa kwa urahisi. Tunawekeza kwenye mifumo bora zaidi ya usalama na vidhibiti vya faragha ambavyo ni rahisi kutumiwa ili uweze kuhifadhi na kushiriki kumbukumbu zako kwa usalama.
Hifadhi salama
Huduma za Google huendelea kulindwa na mfumo wa kina zaidi wa usalama kote duniani. Usalama huu uliojumuishwa hutambua na kuzuia hatari za mtandaoni ili uwe na uhakika kuwa taarifa zako binafsi ni salama.
Usimbaji fiche
Usimbaji fiche hudumisha usalama na faragha ya data inapotumwa. Unapohifadhi picha, data unayotengeneza huhamishwa kati ya kifaa chako, huduma za Google na vituo vyetu vya data. Tunalinda data hii kwa kutumia safu nyingi za usalama, ikiwa ni pamoja na teknolojia bora zaidi ya usimbaji fiche kama vile HTTPS na usimbaji wakati data imehifadhiwa.
Kupanga picha katika makundi kulingana na nyuso za waliomo
Kipengele cha kupanga picha kulingana na nyuso za waliomo huweka kiotomatiki nyuso zinazofanana kwenye kikundi na kukupangia ili kukurahisishia kutafuta na kudhibiti picha zako. Ni wewe tu unayeweza kuona lebo na makundi ya nyuso. Unaweza kudhibiti ikiwa kipengele cha kupanga picha kulingana na nyuso za waliomo kimezimwa au kimewashwa na ukikizima, makundi ya nyuso yatafutwa kwenye akaunti yako. Hatubuni teknolojia yenye madhumuni ya jumla ya utambuzi wa sura kwa lengo la kibiashara. Pata maelezo zaidi.
Mpango wa Washirika
Tunashirikiana kwa karibu sana na washirika na wasanidi programu ambao hutumia API ya programu ya Picha kwenye Google ili kuhakikisha kuwa wanabuni vipengele muhimu ambavyo vinaimarisha hali yako ya utumiaji wa programu ya Picha kwenye Google. Washirika wetu wanahitajika kutii sera zetu na hawawezi kufikia data yoyote bila ruhusa yako.
Hali maalum ya kuhifadhi nakala
Unaweza kuchagua kuhifadhi nakala ya picha na video zako kwenye programu ya Picha kwenye Google au uhifadhi tu nakala za picha ambazo ungependa kuhifadhi kwenye akaunti yako ya Google.
Kumbukumbu
Furahia kumbukumbu zako bora, unazoonyeshwa kwa faragha. Una chaguo la kujiondoa ili usione Kumbukumbu za watu au vipindi fulani, pia una uwezo wa kufunga kipengele hiki.
Mwonekano wa Ramani
Angalia picha zako kulingana na mahali kwenye ramani wasilianifu ambayo ni wewe tu unayeweza kuiona. Mwonekano huu wa ramani huwekwa kwa kutumia data ya mahali iliyohifadhiwa kwenye Akaunti yako ya Google. Unaweza kubadilisha na kuondoa data ya mahali inayotumiwa kuweka ramani katika photos.google.com. Kama hungependa kuona picha zako za baadaye zikiwa zimepangwa kwenye mwonekano huu wa ramani, unaweza kuzima mipangilio ya Kumbukumbu ya Maeneo Yangu na data ya mahali kwenye programu yako ya kamera.
Mratibu wa Google
Uliza programu ya Mratibu wa Google ili ikusaidie upate, uangalie au ushiriki picha. Kwenye mipangilio yako ya programu ya Mratibu, unaweza kuchagua unachotaka kuonyesha na kushiriki kutoka kwenye vifaa vyako vilivyo na programu ya Mratibu, kama vile Google Nest Hub au simu yoyote ya Android. Ili uratibu na kudhibiti picha zinazoonekana kwenye Skrini Mahiri mahususi au vifaa vya kutuma maudhui vilivyounganishwa, unaweza kutumia mipangilio ya kifaa mahususi kwenye programu yako ya Google Home.
Kushiriki albamu
Unaposhiriki albamu, mipangilio chaguomsingi itakuwa ni kushiriki na watu au mtu mahususi kupitia Akaunti yake ya Google. Hatua hii inakupatia uwezo zaidi wa kudhibiti anayeweza kuongezwa kwenye albamu. Bado una chaguo la kushiriki kupitia kiungo, hali ambayo inarahisisha shughuli ya kushiriki picha na watu ambao hawatumii programu ya Picha kwenye Google wala Akaunti ya Google. Unaweza kusasisha mipangilio ya kushiriki albamu zako wakati wowote na kudhibiti anayeweza kufikia kila albamu.
Kushiriki moja kwa moja
Unaposhiriki picha na video za mara moja, utakuwa na chaguo la kuziongeza kwenye mazungumzo ya faragha yanayoendelea kwenye programu.
Shughuli za kushiriki
Kila kitu ambacho umeshiriki kupitia programu ya Picha kwenye Google kinapatikana mahali pamoja ili uweze kupata picha zote ambazo umeshiriki na familia na marafiki zako.
programu ya Picha kwenye Google.