Barua pepe ambayo
hulinda usalama wa taarifa zako za faragha.
Gmail hujitahidi kukulinda dhidi ya barua taka, wizi wa data binafsi na programu hasidi, kabla hazijafikia kikasha chako. Uwezo wetu wa kuchuja barua taka, ulioboreshwa kwa utashi wa kompyuta huzuia takribani barua pepe taka milioni 10 kila dakika.
Ulinzi dhidi ya wizi wa data binafsi
Ulinzi dhidi ya wizi wa data binafsi
Mashambulizi mengi ya programu hasidi na ya wizi wa data binafsi huanza kwa barua pepe. Gmail huzuia zaidi ya asilimia 99.9 ya barua taka, majaribio ya wizi wa data binafsi na programu hasidi dhidi ya kukuathiri.
Kuvinjari Salama
Kuvinjari Salama
Kipengele cha Kuvinjari Salama hukulinda kwa kutambua viungo hatari kwenye ujumbe wa barua pepe na kukuonya kabla hujatembelea tovuti.
Arifa zinazotumwa kiotomatiki
Arifa zinazotumwa kiotomatiki
Gmail hukuonya kabla hujapakua kiambatisho ambacho kinaweza kuhatarisha usalama wako.
Usalama wa akaunti
Usalama wa akaunti
Tunalinda akaunti yako dhidi ya shughuli za kuingia katika akaunti zinazotiliwa shaka na zile ambazo hazijaidhinishwa kwa kufuatilia viashiria kadhaa vya usalama. Pia tunatoa Mpango wa Ulinzi wa Hali ya Juu kwa akaunti zilizo katika hatari kubwa ya mashambulizi mahususi.
Hali ya siri
Hali ya siri
Unaweza kufanya ujumbe wako utoweke baada ya kipindi fulani na uondoe chaguo la wapokeaji kusambaza, kunakili, kupakua au kuchapisha ujumbe wako kwenye Gmail.
Usimbaji wa barua pepe
Usimbaji wa barua pepe
Kwenye mfumo wa Google, ujumbe husimbwa ukiwa umehifadhiwa na unapotumwa kati ya vituo vya data. Ujumbe unaotumwa kwa watoa huduma wengine husimbwa na mbinu ya Transport Layer Security panapowezekana au inapohitajika na mipangilio.