Kukusaidia kuweka
sheria dijitali za msingi kwa kutumia Family Link.
Family Link hukusaidia kudhibiti akaunti na vifaa vya watoto wako wanapotumia mtandao. Unaweza kudhibiti programu, kufuatilia muda wa kutumia kifaa na kusaidia kuweka sheria dijitali za msingi kwa ajili ya familia yako.
-
Ripoti za shughuli kwenye programu
Muda wa kutumia kifaa hutofautiana. Unaweza kutegemea iwapo mtoto wako anatumia kifaa kusoma kitabu, kutazama video au kucheza michezo ya video. Unaweza pia kutumia ripoti za shughuli za programu ya Family Link kubaini programu ambazo mtoto wako anatumia zaidi na ufanye uamuzi kuhusu anachoweza kufikia.
-
Muda wa kutumia kila siku
Utaamua muda ambao mtoto wako anapaswa kutumia kifaa. Family Link hukuruhusu kuweka kipimo cha muda wa kila siku wa kutumia kifaa, kuweka wakati wa kulala kwenye kifaa na kufunga kifaa cha mtoto wako cha Android au cha mfumo wa uendeshaji wa Chrome ukiwa mbali.
-
Dhibiti maudhui na ununuzi
Idhinisha au kataza upakuaji wa programu kutoka kwenye Duka la Google Play na ununuzi wa ndani ya programu ambao mtoto wako angependa kufanya.
Dhibiti mipangilio ya akaunti
Kudhibiti na kudumisha usalama wa akaunti ya mtoto wako
Fikia Vidhibiti vya Shughuli vya mtoto wako kwenye mipangilio ya Family Link. Kama mzazi, unaweza kusaidia kubadilisha au kuweka upya nenosiri la mtoto wako iwapo amelisahau. Pia unaweza kubadilisha taarifa binafsi za mtoto wako au ufute akaunti yake ikiwa utahitaji kufanya hivyo. Hawezi kuongeza wasifu mwingine kwenye akaunti au kifaa chake bila ruhusa yako. Pia, unaweza kuangalia mahali kilipo kifaa chake cha Android (mradi kimewashwa, kimeunganishwa kwenye intaneti na kimetumika hivi majuzi).
Kwa usaidizi kuhusu sheria dijitali za msingi za familia, angalia Mwongozo wetu wa Familia. Ukiwa na vidokezo vya kuanzisha mazungumzo kuhusu teknolojia na watoto wako, wewe na familia yako mnaweza kuvinjari mtandaoni pamoja kwa uhakika zaidi.
-
Ruhusu mtoto wako afikie programu ya Mratibu wa Google kupitia akaunti inayodhibitiwa
Watoto wanaweza kuingia katika akaunti ya vifaa vinavyoweza kutumia programu ya Mratibu wa Google wakitumia akaunti yao, inayodhibitiwa na Family Link. Wanapata hali inayofaa ya kutumia programu ya Mratibu na wanaweza kufikia hadithi, matukio na michezo inayolenga familia yote. Watoto wanazuiliwa wasifanye ununuzi wowote. Wazazi wanaweza kuamua iwapo watoto wao watapata idhini ya kufikia programu za watu au kampuni nyingine kwenye programu ya Mratibu.
-
Dhibiti idhini ya mtoto wako ya kufikia tovuti kwenye Chrome
Unaweza kudhibiti idhini ya mtoto wako ya kufikia tovuti mahususi wakati anatumia kivinjari cha Chrome kwenye kifaa chake cha mfumo wa uendeshaji wa Android au Chrome. Unaweza kuchagua kudhibiti tovuti ambazo unataka mtoto wako afikie au uzuie tovuti mahususi ambazo hutaki atembelee.
-
Chuja matokeo ya maudhui machafu kwenye huduma ya Tafuta
Ili upate safu ya ziada ya usalama, unaweza kuwasha Utafutaji Salama ili kusaidia kuchuja matokeo yenye maudhui machafu, kama vile ponografia. Utafutaji Salama huwashwa kwa chaguo msingi kwa watumiaji wanaoingia katika akaunti, walio na umri wa chini ya miaka 13 (au umri husika katika nchi uliko) ambao akaunti zao zinadhibitiwa na Family Link. Wazazi pia wana chaguo la kuzima au kuzuia uwezo wa kufikia huduma ya Tafuta.