Kubuni hali za utumiaji zinazofaa familia.
Tunabuni vipengele maalum – kama vile vichujio mahiri, vizuia tovuti na ukadiriaji wa maudhui – kwenye baadhi ya bidhaa zetu ili kuzifanya ziridhishe zaidi familia yako.
maudhui ya kusaidia watoto
kugundua, kubuni na kukua.*
-
Imebuniwa kwa kuzingatia udadisi wa watoto
Iwe ni miradi ya wanyama au sanaa, watoto huwa wataalamu wadogo kuhusu mambo wanayopenda. Ndiyo maana Kids Space inapendekeza maudhui bora kwa watoto wako kulingana na mambo yanayowavutia wanayochagua. Kwa kutumia maudhui yaliyopendekezwa, watoto wanaweza kugundua mambo yanayowavutia sasa kwa njia mpya zinazowashirikisha. Watoto wanaweza pia kuweka mapendeleo kwenye hali yao ya utumiaji kwa kubuni mhusika wao mwenyewe.
-
Programu, vitabu na video zinazopendekezwa
Mtoto anapofungua Kids Space, ataona maktaba ya maudhui bora. Watoto wanaweza kugundua mapendekezo ya programu, michezo, vitabu na video ili kupata mbinu mpya za kucheza na kujifunza.†
-
Weka mipaka kwa kutumia vidhibiti vya wazazi
Kwa kutumia vidhibiti vya wazazi katika Family Link unaweza kuelekeza hali ya utumiaji ya mtoto wako kwa kudhibiti maudhui, kuweka vipimo vya muda wa kutumia kifaa na zaidi, yote haya kwenye kifaa chako mwenyewe.
YouTube Kids
Gundua ulimwengu wa mafunzo na burudani ukitumia YouTube Kids
Tumebuni YouTube Kids iwe huduma salama kwa ajili ya watoto ili wagundue mambo yanayowavutia kupitia video za mtandaoni. Unaweza kupata video zinazofaa familia zinazoangazia mada zote tofauti kwenye vifaa vyako vyote, iwe umepakua programu ya YouTube Kids, kututembelea kwenye wavuti au kutazama YouTube Kids katika televisheni yako inayoweza kuunganisha kwenye intaneti.
Google Play
Maudhui “yaliyoidhinishwa na walimu” kwa ajili ya mtoto wako kwenye Google Play
Tunashirikiana na wataalamu wa elimu na walimu kote nchini, ili kukusaidia kupata maudhui ambayo ni sahihi kwa watoto wako. Vinjari kichupo chetu cha Watoto kwenye Duka la Google Play ili upate programu “zilizoidhinishwa na Walimu” ambazo hufunza na kuburudisha. Kwenye ukurasa wa programu wa maelezo, unaweza kuona kwa nini walimu huzipa programu ukadiriaji wa kiwango cha juu na uangalie ukadiriaji wa maudhui ili uelewe iwapo programu inafaa kwa umri wa watoto. Unaweza pia kuona kama programu ina matangazo, inaruhusu ununuzi wa ndani ya programu au inahitaji ruhusa za kifaa.
Tunawasimamia wasanidi programu wanaobuni programu za watoto katika kiasi kikubwa kwa kutumia sera zetu za wasanidi programu za Duka la Google Play.
Mratibu wa Google
Furaha kwa familia yote kwa usaidizi kutoka kwenye programu ya Mratibu wa Google
Programu yako ya Mratibu hurahisisha hatua ya kupata burudani ya familia yote ili mfurahie pamoja. Gundua michezo na shughuli zinazofaa familia, iliyobuniwa kupitia mpango wetu wa Vitendo Vinavyolenga Familia au sikiliza hadithi unazopenda kabla ya kulala kwa kuiambia tu programu ya Mratibu wako ikusimulie hadithi. Sikiza muziki ambao familia nzima inaweza kufurahia baada ya kuweka Vichujio na utumie Wakati wa kupumzika kwenye kifaa chako ili kusitisha na kunufaika na muda wenyu pamoja.
Wataalamu wamekagua shughuli zetu zote za Vitendo Vinavyolenga Familia ili kubaini ufaafu kwa familia, lakini hakuna mfumo usio na kasoro. Maudhui yasiyofaa yanaweza kupatikana, kwa hivyo tunajitahidi kuboresha kinga zetu.
Google Workspace
Kubuni mazingira salama zaidi ya mafunzo kwenye madarasa
Google Workspace for Education huwasaidia walimu na wanafunzi wawasiliane kwa njia salama kwenye vifaa vyote. Huduma zake za msingi hazijumuishi matangazo na hatutumii taarifa zozote binafsi za watumiaji katika shule za msingi na za upili (K–12) kuwaonyesha matangazo. Pia, tunatoa zana za kuwasaidia wasimamizi waweke sera kuhusu shughuli zinazofaa na kusaidia kuwalinda wanafunzi wanaotumia Akaunti za Google shuleni. Tumejitolea kuzipa shule zana na nyenzo zinazohitaji ili kufanya uamuzi wa busara kuhusu huduma za Google Workspace for Education zinazotumiwa na wanafunzi.
Chromebook
Kufanya darasa liwe salama
Mamilioni ya wanafunzi wanatumia Chromebook – kompyuta za kupakata za Google – madarasani. Wasimamizi wanaweza kudhibiti mipangilio ya makundi ili kuwapa wanafunzi utendaji au uwezo wanaohitaji. Vipengele vyetu vya faragha na usalama husaidia kulinda taarifa binafsi ya watoto na vimesaidia kufanya Chromebook iwe chaguo bora Marekani katika shule za K–12 na shule nyingi katika nchi zingine.
* Google Kids Space inahitaji Akaunti ya Google ya mtoto wako. Ili uweze kutumia vidhibiti vya wazazi, unahitaji kusakinisha programu ya Family Link kwenye kifaa cha Android, Chromebook au iOS kinachoweza kutumika.
† Maudhui ya vitabu na video hayapatikani katika maeneo yote. Maudhui ya video yanategemea upatikanaji wa programu ya YouTube Kids. Maudhui ya vitabu yanahitaji programu ya Vitabu vya Google Play. Upatikanaji wa programu, vitabu na maudhui ya video unaweza kubadilika bila ilani. Programu ya Mratibu wa Google haipatikani katika Google Kids Space.