Ikifanya kazi kuhusu usalama wa mtandaoni katika eneo la Málaga.

Ikiwa katikati ya eneo la Andalusia, GSEC Málaga ni kituo cha kimataifa kinachohusu usalama wa mtandaoni ambapo wataalamu wa Google hufanya kazi kuelewa mazingira ya vitisho vya mtandaoni na kubuni zana zinazodumisha usalama zaidi wa biashara, serikali na watumiaji mtandaoni

Kuangazia zaidi mikakati yetu ya usalama wa mtandaoni.

GSEC Málaga ni kituo kikuu cha usalama wa mtandaoni cha Google barani Ulaya. Timu zetu zinashirikiana na serikali za Ulaya, biashara na wataalamu ili kudumisha zaidi usalama wa watu mtandaoni, kuendeleza ujuzi wa dijitali na kubuni zana za kupambana na vitisho tata vya mtandaoni vinavyozidi kuongezeka.

Dirisha la kivinjari likionyesha kielelezo cha zana ya kuchanganua programu hasidi ya VirusTotal.

TAARIFA KUHUSU VITISHO

Kujenga uelewa kuhusu usalama wa mtandaoni

GSEC Málaga hufanya kazi kama kituo cha ushirikiano kuhusu desturi bora, utafiti na maarifa, kuwakutanisha pamoja wataalamu wa Google ili wafanye kazi pamoja na watunga sera, wasomi na biashara za Ulaya ili kuongeza uelewa wetu wa pamoja wa mazingira ya vitisho vya mtandaoni na kuboresha ujuzi wa usalama wa mtandaoni na utaalamu kote barani Ulaya.

Dirisha la kivinjari likionyesha kidhahania zana ya kugundua tishio ya Chronicle.

SHUGHULI ZA USALAMA

Utambuzi wa vitisho na hatua zinazochukuliwa

GSEC Málaga huwaleta pamoja wataalamu na timu mbalimbali za Google kufanya kile wanachofanya vizuri zaidi: kuunda na kuimarisha zana za kisasa na utafiti mpya kabisa. Zikishirikiana, timu za Google ikiwa ni pamoja na VirusTotal, Mandiant na Shughuli za Usalama za Google hufanya utafiti na kubuni zana za kukulinda dhidi ya vitisho tata vinavyozidi kuongezeka na watendaji hasidi - kwa msingi wa kasi, programu huria na Akiliunde (AI).

Wafahamu watu wanaohusika na GSEC Málaga.

Timu ya Kituo cha Uhandisi wa Usalama kwenye Google ina wataalamu wa usalama wa mtandaoni kutoka Hispania na kote barani Ulaya ambao wamejikita katika kujenga mazingira salama zaidi ya Intaneti.

Picha ya sura ya Bernardo Quintero

“Google ina historia ya muda mrefu ya kufanya kazi ya kudumisha usalama wa watu mtandaoni na GSEC Málaga huchangia kwenye dhamira hii ya kufanya Intaneti iwe sehemu salama zaidi.”

Bernardo Quintero

Founder, VirusTotal

Picha ya sura ya Ángela Casal Bernardini

“Tunabuni mfumo wa usalama ambapo kila mtu huchangia na hunufaika.”

Ángela Dini

Head of Design, VirusTotal

Picha ya sura ya Emiliano Martinez

“Tunajenga uelewa kuhusu mashambulizi ya mtandaoni na mifumo ya washindani. Hali hii huturuhusu kuwezesha mashirika kukabiliana na vitisho na kulinda kwa uthabiti data, wafanyakazi, watumiaji na biashara yake.”

Emiliano Martinez

Lead Product Manager, VirusTotal

Picha ya sura ya Marta Gómez

“Ninabuni masuluhisho ya usalama wa mtandaoni yanayotumiwa na watu kujilinda dhidi ya wahalifu wa mtandaoni.”

Marta Gómez

Software Engineer

Picha ya sura ya Juan Infantes

“Dhamira yetu ni kubuni mazingira salama zaidi ya utumiaji wa intaneti kwa familia, biashara na serikali kote barani Ulaya na duniani.”

Juan Infantes

Tech Lead, VirusTotal

Picha ya sura ya Paloma Simon

“Hapa GSEC Malaga, tunaipatia jumuiya uelewa, kwa kutumia kikundi chetu kama jukwaa la ushiriki wa masuala ya mtandaoni katika ngazi zote.”

Paloma Simon

GSEC Malaga Program Manager

Picha ya sura ya Karl Hiramoto

“Ili kudumisha usalama wa watumiaji mtandaoni, VirusTotal hupanga taarifa za ulimwenguni zinazohusu faili na URL hasidi na huzifanya zifae na ziweze kufikiwa ulimwenguni.”

Karl Hiramoto

Senior Software Engineer

Picha ya sura ya Vicente Díaz

"Lengo letu ni kusaidia watu kuwa salama mtandaoni kwa kufanya taarifa kuhusu vitisho ziweze kutekelezwa, kueleweka na ziwafae kadiri iwezekanavyo"

Vicente Díaz

Software Engineer

Uboreshaji wa usalama mtandaoni

Pata maelezo kuhusu jinsi tunavyohakikisha usalama wa watu wengi zaidi mtandaoni kuliko mtu mwingine yeyote duniani.