Kushughulikia suala la uwajibikaji wa maudhui jijini Dublin.

Kituo cha kimaeneo cha wataalamu wa Google, GSEC Dublin, kinapatikana katika makao makuu yetu ya Ulaya. Kituo hiki hujitahidi kukabiliana na matukio ya kusambazwa kwa maudhui haramu na hatari. Ni eneo ambako tunaweza kushiriki kazi hii na watunzi wa sera, watafiti na wadhibiti.

Kuangazia mikakati yetu ya uwajibikaji wa maudhui.

Dublin ni kitovu cha timu zetu zinazoshughulikia masuala ya Uaminifu na Usalama, zinazojumuisha wataalamu wa sera, wataalamu maalum na wachanganuzi wanaofanya kazi ili kulinda usalama wa watu mtandaoni kwa kutumia teknolojia mpya zaidi na utashi wa kompyuta. Mikakati hii inatoa maelezo ya ziada ya uwazi katika kazi yao.

YouTube Inavyofanya Kazi

Maelezo kuhusu sera, bidhaa na hatua tunazochukua

Kila siku, mamilioni ya watu hutembelea YouTube ili kupata habari, kuhamasishwa au kuburudishwa. Kwa muda mrefu, maswali yameulizwa kuhusu jinsi YouTube inavyofanya kazi, kwa hivyo tumebuni tovuti hii ili kutoa baadhi ya majibu – na kufafanua tunachofanya ili kubuni mfumo unaowajibika na ambao unaweza kutegemewa na watumiaji, watayarishi na wasanii katika jumuiya yetu.

Zana za Usalama wa Watoto

Kukabiliana na maudhui ya dhuluma na unyanyasaji wa watoto mtandaoni

Google imejitolea kukabiliana na maudhui yanayoonyesha unyanyasaji wa watoto kingono (CSAM) mtandaoni na kuzuia mifumo yetu isitumiwe kusambaza maudhui ya aina hii. Tunawekeza zaidi katika masuala ya kukabiliana na unyanyasaji wa watoto mtandaoni na tunatumia teknolojia tunayomiliki ili kutambua, kuzuia na kuondoa maudhui yasiyofaa kwenye mifumo yetu. Tunatumia pia utaalamu wetu wa kiufundi ili kubuni na kushiriki zana za kusaidia mashirika mengine yatambue na kuondoa maudhui yanayoonyesha unyanyasaji wa watoto kingono kwenye mifumo yao.

Ripoti ya Uwazi

Kushiriki data kuhusu ufikiaji wa habari

Tangu mwaka wa 2010, Google imeshiriki Ripoti ya Uwazi mara kwa mara ili kusaidia kufafanua jinsi sera na hatua zinazochukuliwa na serikali na mashirika mbalimbali huathiri faragha, usalama na ufikiaji wa habari. Tovuti yetu ya Ripoti ya Uwazi inajumuisha data kuhusu maombi ya kuondolewa kwa maudhui kutoka kwa serikali, uondoaji wa maudhui kwa sababu za hakimiliki, utekelezaji wa Mwongozo wa Jumuiya ya YouTube na utangazaji wa maudhui ya kisiasa kwenye Google na zaidi.

Kutana na watu wanaofanikisha mikakati ya kitovu cha GSEC Dublin.

Timu ya Kituo cha Uhandisi wa Usalama kwenye Google ina mamia ya wachanganuzi, wahandisi, wataalamu wa sera, watafiti na wataalamu wengine, wanaofanya kazi ili kuhakikisha intaneti iliyo bora na salama.

Amanda Storey

“Kitovu cha GSEC Dublin kitafanya iwe rahisi kwa wadhibiti, watunzi wa sera na watafiti kupata ufahamu halisi kuhusu jinsi tunavyoshughulikia suala la usalama wa maudhui.”

Amanda Storey

DIRECTOR OF TRUST & SAFETY

Helen O’Shea

“Dhamira yetu ni kulinda watu wanaotumia bidhaa zetu, watuamini sisi, washirika wetu na jumuiya ambako tunahudumu. Pia kusaidia Google ifanikiwe katika kukabiliana na matumizi mabaya na watendaji wabaya.”

Helen O’Shea

HEAD OF CONTENT RISK & COMPLIANCE

Mary Phelan

“Mfumo wetu wa michakato yenye utaratibu huturuhusu tusaidie watu kupata habari zinazoaminika kutoka kwa vyanzo vya kitaalamu, huku pia tukilinda watumiaji wetu dhidi ya maudhui ambayo ni dhahiri kuwa ni hatari na yenye madhara.”

Mary Phelan

DIRECTOR OF TRUST & SAFETY

Picha ya Claire Lilley

"Kila siku, timu zetu hujitahidi kutafuta suluhu kuhusu jinsi ya kuwezesha ufikiaji wa habari kwenye mifumo yetu huku pia zikilinda mifumo hiyo na watu wanaoitumia dhidi ya madhara na matumizi mabaya... yaani madhara ya mtandaoni na yanayoweza kutokea nje ya mtandao."

Claire Lilley

CHILD ABUSE ENFORCEMENT MANAGER

Picha ya Brian Crowley

"Kupitia kitovu cha GSEC, wadhibiti wataweza kufikia habari zaidi kuhusu jinsi mifumo yetu ya udhibiti wa maudhui na teknolojia zingine hutumiwa kwa njia halisi, katika eneo salama ambalo hulinda usiri wa taarifa za watumiaji."

Brian Crowley

DIRECTOR OF GLOBAL ADS AND CONTENT INVESTIGATIONS

Picha ya Nuria Gómez Cadahía

"Katika suala la maudhui kwenye mifumo yetu, tuna wajibu wa kulinda usalama wa watu na biashara zinazotumia bidhaa zetu, na kufanya hivyo kwa kutumia michakato na sera zinazoeleweka kwa uwazi."

Nuria Gómez Cadahía

TECHNICAL PROGRAM MANAGER

Picha ya Ollie Irwin

"Dublin ni kitovu cha timu zetu zinazoshughulikia masuala ya Uaminifu na Usalama katika eneo hilo, zinazojumuisha wataalamu wengi tofauti wa masuala ya faragha, wataalamu maalum na wahandisi wanaofanya kazi ili kulinda usalama wa watu mtandaoni kwa kutumia teknolojia mpya zaidi na utashi wa kompyuta."

Ollie Irwin

STRATEGIC RISK MANAGER

Nyuma ya pazia
katika Kituo cha Uhandisi wa Usalama kwenye Google.

Tunaongea na watumiaji duniani kote kuelewa maswala yao kuhusu usalama wa Intaneti. Tunapatia timu ya wahandusi wetu nafasi, msukumo na usaidizi kutengeneza suluhu za kizazi kijacho kusaidia kuimarisha usalama mtandaoni.

Uboreshaji wa usalama mtandaoni

Pata maelezo kuhusu jinsi tunavyohakikisha usalama wa watu wengi zaidi mtandaoni kuliko mtu mwingine yeyote duniani.