Mfumo Salama wa AI ya Google (SAIF)
Uwezo wa AI, hasa AI zalishi, ni mkubwa. Kadiri uvumbuzi unavyoongezeka, sekta hii inahitaji viwango vya usalama vya kujenga na kutumia AI kwa kuwajibika. Ndio maana tulianzisha Secure AI Framework (SAIF), mfumo wa dhana wa kulinda mifumo ya AI.
SAIF imeundwa kushughulikia maswala maarufu ya wataalamu wa usalama, kama vile faragha, usalama na udhibiti wa hatari katika miundo ya AI/Mashine Kujifunza (ML), hatua inayosaidia kuhakikisha kuwa miundo ya AI inapotekelezwa, huwa salama kwa chaguomsingi.
Tunafurahi kusambaza hatua za kwanza katika safari yetu ya kubuni mfumo ikolojia wa SAIF kwa serikali, biashara na mashirika ili kuboresha mfumo wa matumizi salama ya AI unaowafaa wote.
Kuwezesha SAIF katika serikali na mashirika
Tunashirikiana na serikali pamoja na mashirika ili kusaidia kupunguza hatari za usalama wa AI. Kazi yetu na watunga sera na mashirika ya viwango, kama vile NIST, huchangia katika kuendeleza mifumo ya udhibiti. Hivi majuzi tuliangazia jukumu la SAIF katika kulinda mifumo ya AI, tukizingatia juhudi za AI za Ikulu ya Marekani.
Kupanua SAIF kupitia washirika wa sekta
Tunapokea usaidizi kuhusiana na SAIF kutoka kwa washirika na wateja katika sekta, kuandaa warsha za SAIF na wataalamu na kuchapisha mbinu bora za usalama za AI. Tulishirikiana na Deloitte katika ripoti rasmi kuhusu jinsi mashirika yanavyoweza kutumia AI kushughulikia changamoto za usalama.
-
Android: Mwongozo wa Usanidi Salama
Linda shirika lako ukitumia arifa za uwezekano wa kuathirika i realtid na ufuate mwongozo salama wa usanidi wa msimbo wa (Mashine Kujifunza) ML
Je, SAIF na AI inayowajibika vinahusiana vipi?
Google ina wajibu wa kubuni AI kwa kuwajibika na kuwawezesha wengine kufanya vivyo hivyo. Kanuni zetu za AI, zilizochapishwa mwaka wa 2018, zinaelezea dhamira yetu ya kuendeleza teknolojia kwa kuwajibika na katika namna iliyoundwa kwa usalama, inayowezesha uwajibikaji na kudumisha viwango vya juu vya ubora wa kisayansi. AI inayowajibika ni mbinu yetu kuu ambayo ina vipimo kadhaa kama vile 'Usawa', 'Ufafanuzi', 'Usalama' na 'Faragha' ambavyo huongoza michakato yote ya utengenezaji wa bidhaa za AI ya Google.
SAIF ni mfumo wetu wa kubuni mbinu sanifu na kamili ya kuunganisha hatua za usalama na faragha katika programu zinazowezeshwa na (Mashine Kujifunza) ML. Inalingana na vipimo vya 'Usalama' na 'Faragha' vya kubuni AI kwa kuwajibika. SAIF inahakikisha kwamba programu zinazowezeshwa na ML zinatengenezwa kwa kuwajibika, kwa kuzingatia ukuaji wa upeo wa vitisho na matarajio ya mtumiaji.
Google inatekelezaje SAIF?
Google ina historia ya muda mrefu ya kukuza AI inayowajibika na kuongeza usalama mtandaoni, na tumekuwa tukiambatisha mbinu bora za usalama kwenye uvumbuzi mpya wa AI kwa miaka mingi. Mfumo wetu Salama wa AI umetokana na uzoefu na mbinu bora zaidi tulizounda na kutekeleza. Pia huonyesha mbinu ya Google ya kusanidi programu zinazowezeshwa na ML pamoja na AI zalishi, zenye ulinzi unaoweza kubadilika, endelevu na nyumbufu unaotumika katika michakato ya usalama na faragha. Tutaendelea kukuza na kujenga SAIF ili kushughulikia hatari mpya, mabadiliko ya upeo na maboresho ya AI.
Je, wataalamu wanaweza kutekeleza vipi mfumo huo?
Angalia mwongozo wetu wa haraka wa kutekeleza mfumo wa SAIF
-
Hatua ya 1 - Kuelewa matumizi
- Kuelewa tatizo mahususi la biashara ambalo AI itasuluhisha na data inayohitajika ili kufunza muundo huo, kutasaidia kuendeleza sera, itifaki na vidhibiti vinavyohitaji kutekelezwa kama sehemu ya SAIF.
-
Hatua ya 2 - Tengeneza timu
- Kubuni na kutumia mifumo ya AI, kama mifumo ya asili, ni juhudi za fani nyingi.
- Mifumo ya AI mara nyingi huwa changamano na si bayana, ina idadi kubwa ya vipengee, inategemea kiasi kikubwa cha data, inatumia rasilimali nyingi, inaweza kutumika kutekeleza maamuzi yanayotegemea maoni na inaweza kuzalisha maudhui mapya yanayoweza kukera, kudhuru au yanayoweza kuendeleza mila potofu na upendeleo katika kijamii.
- Anzisha timu inayofaa ya utendaji ili kuhakikisha kuwa masuala ya usalama, faragha, hatari na kutii vinajumuishwa toka mwanzo.
-
Hatua ya 3 - Kiwango kilichowekwa na AI Primer
- Wakati timu zinapoanza kutathmini matumizi ya biashara, matatizo mbalimbali na yanayokua, hatari na vidhibiti vya usalama vinavyotumika - ni muhimu kwamba vikundi vinavyohusika vielewe mambo msingi katika kipindi cha kubuni muundo wa AI, usanifu na mantiki ya mbinu za muundo, ikiwa ni pamoja na uwezo, manufaa na mapungufu.
-
Hatua ya 4 - Tumia vipengele sita vya msingi vya SAIF (vilivyoorodheshwa hapo juu)
- Vipengele hivi havijakusudiwa kutumika katika mpangilio wa matukio.
Je, ninaweza kupata wapi maelezo zaidi kuhusu SAIF na jinsi ya kuitumia katika biashara au asasi yangu?
Endelea kufuatilia! Google itaendelea kuunda na kutuma rasilimali, mwongozo na zana za Mfumo Salama wa AI, pamoja na mbinu nyingine bora katika utayarishaji wa programu za AI.
Kama mojawapo ya kampuni za kwanza kuelezea kuhusu Al principles, tumeweka kiwango cha responsible Al. Kiwango hiki huongoza utengenezaji wa bidhaa zetu zinazotumika katika usalama. Tumetetea na kuendeleza mifumo ya sekta ili kuinua kiwango cha usalama na kujifunza kwamba kujenga jamii ili kuboresha kazi ni muhimu ili kuwa na mafanikio kwa kipindi kirefu. Ndiyo maana tunafurahi kujenga jamii ya SAIF inayomfaa kila mtu.