Kila siku Google hufanya kazi kuhakikisha kuwa intaneti ni salama kwa kila mtu
Kulinda watu, biashara na serikali
Usalama ni nguzo ya mkakati wetu wa bidhaa. Ndio maana bidhaa zetu zote zina ulinzi uliojumuishwa ambao unafanya ziwe salama kwa chaguomsingi.
Pata maelezo zaidiKuiwezesha jamii kushughulikia hatari za usalama mtandaoni
Tunaiwezesha jamii kutumia uwezo wa programu huria na kushiriki maarifa na utaalamu wetu na sekta kwa uwazi ili kuifanya mifumo iwe salama.
Pata maelezo zaidiBoresha teknolojia za siku zijazo
Tunataka kulinda jamii dhidi ya kizazi kijacho cha vitisho vya mtandaoni. Kuimarisha utaalamu wetu wa AI, tunabuni awamu ijayo ya usanifu utakaovuka mipaka ya ubunifu wa usalama.
Pata maelezo zaidiTunabuni ulinzi ulioboreshwa katika kila hatua ya uundaji wetu wa bidhaa na miundombinu ya wingu. Hatua hii inawezesha mashirika kuwa ya kisasa na kuimarisha ulinzi wao wa TEHAMA huku wakisaidia watumiaji kulinda taarifa zao binafsi na kufikia Intaneti kwa usalama.
-
Kupambana na maudhui hatari
Tunazuia matumizi mabaya na kuwalinda watumiaji, hasa watoto kwa kutambua na kuondoa maudhui hatari yaliyo kinyume na sheria, yanayokiuka sera zetu. Tunafanya hivi kwa aina zote za madhara, ikiwemo matangazo yanayopotosha, taarifa za kupotosha, chuki, ulaghai na usalama wa watoto.
Tunashirikiana na viongozi wa usalama mtandaoni, serikali na jumuiya za usalama ili kuboresha viwango vya kimataifa vinavyotoa kipaumbele kwa ulinzi wa mtumiaji, vinapambana na taarifa za kupotosha na kushiriki taarifa za vitisho ili kuifanya Intaneti iwe wazi na salama kwa kila mtu.
-
Kuimarisha wanaofanya kazi mtandaoni
Tunawawezesha wafanyakazi wa mtandaoni kwa kushiriki utaalamu wetu, kupanua nafasi za kazi na kuunda ushirikiano imara ndani ya sekta na serikalini ili kusaidia upatikanaji wa ajira zaidi katika tasnia ya usalama mtandaoni — bila kujali uzoefu au historia — na kujenga dunia iliyo salama kwa wote.
-
Mandiant Threat Intelligence
Mandiant inakuletea taarifa za kina za vitisho, katika wakati halisi zilizopatikana kutoka sehemu za kuaminika za usalama mtandaoni pamoja na mashirika makubwa zaidi duniani. Ikijumuishwa na usalama wa Wingu la Google, tunasaidia biashara na taasisi za sekta za umma kuwa salama katika kipindi chote cha ulinzi.
Tunashughulikia kuhakikisha usalama wa watumiaji walio kwenye hatari ya kushambuliwa mtandaoni huku tukilinda faragha yao kupitia maboresho ya AI, maunzi, matumizi ya kompyuta kwenye wingu na kuweka viwango vya kimataifa vya matumizi ya kompyuta kwa njia ya kwanta.
-
Bidhaa salama zinazowezeshwa na AI
Ulinzi wa kiotomatiki umejumuishwa ndani ya bidhaa zetu ili kuwapa watumiaji wetu wote hali ya utumiaji iliyo salama. Mashine kujifunza husaidia Gmail kuzuia taka, wizi wa data binafsi na programu hasidi kutokea kwenye kikasha chako kwa usahihi wa zaidi ya asilimia 99.9.
-
Maunzi inayoaminika
Funguo za usalama zinatumia kriptografia ya ufunguo wa umma kuhakikisha ulinzi thabiti wa akaunti. Funguo za Usalama za Titan zimejumuishwa na chipu ya maunzi iliyobuniwa kuzuia wizi wa data binafsi na mashambulizi yanayolenga kudondoa programu dhibiti na maudhui ya ufunguo wa siri.
Usalama wa mtandaoni ni shughuli ya kushirikiana, na tunapofanya kazi pamoja, tunaweza kuchochea ubunifu na kubuni mbinu bora zinazowanufaisha wote kwenye mazingira haya magumu, yanayobadilika mara kwa mara.
Timu zetu zinafanya kazi katika nyanja za faragha, usalama, uwajibikaji wa maudhui na usalama wa familia kote duniani. Kituo chetu cha Uhandisi wa Usalama kwenye Google kinasaidia kuongoza kazi hii, inayoongozwa na wahandisi, wataalamu wa sera na maudhui wenye uzoefu.
Jumuiya yetu ya kimataifa ya Bug Hunters inatathmini kwa kina bidhaa zetu ili kuzifanya ziendelee kufanya kazi kwa namna inayotakiwa na kufanya intaneti kuwa mahali salama zaidi.
Tunatumia timu bora zaidi ya ushauri wa ulinzi ili kutegemeza mabadiliko ya dijitali na usalama ya serikali, miundombinu muhimu, biashara na biashara ndogo ndogo.
kuimarisha usalama wako mtandaoni.
-
Kwenye bidhaa zetuPata maelezo kuhusu jinsi usalama wako hulindwa kwenye bidhaa zote za Google.
-
Usalama na faraghaPata maelezo kuhusu jinsi Google hulinda taarifa zako za faragha na kukupatia uwezo wa kuzidhibiti.
-
Usalama wa maudhuiPata maelezo kuhusu jinsi tunavyowasilisha maelezo ya kuaminika ili kuhakikisha intaneti ni salama kwa wote.
-
Usalama wa familiaPata maelezo kuhusu jinsi Google inavyokusaidia udhibiti maudhui yanayofaa familia yako mtandaoni.