Njia salama zaidi ya kuingia katika akaunti zako zote za mtandaoni.
Mchakato wa kuingia katika akaunti zako zote za mtandaoni haupaswi kuwa mgumu. Unapaswa kuwa wa haraka na rahisi bila kukutia wasiwasi kwamba taarifa binafsi za akaunti yako zinaweza kuwa hatarini.
Zana zetu za uthibitishaji zilizojumuishwa zimebuniwa ili kukusaidia uingie katika akaunti kwenye huduma na programu uzipendazo kwa haraka na kwa njia salama.
-
Njia rahisi na salama ya kuingia katika akaunti, bila manenosiri
Funguo za siri hukuwezesha kuingia katika akaunti kwa njia rahisi na salama zaidi kwa kutumia mbinu ya kufunga skrini ya kifaa chako, na hivyo kufanya kuingia katika akaunti iwe rahisi kama ilivyo kuangalia simu yako au kuchanganua alama yako ya kidole. Funguo za siri zinatoa mwongozo kwenye sekta na zinatumika kwenye vifaa na mifumo yako yote.
Pata maelezo zaidi -
Kuingia katika akaunti kwa urahisi kwenye vifaa vyako vyote
Huhitaji kukumbuka au kuandika funguo za siri. Badala yake, unatumia alama ya kidole, kipengele cha kuchanganua uso, PIN au mbinu nyingine ya kufunga skrini kuingia katika akaunti kwa kasi ya mara mbili zaidi ikilinganishwa na kutumia nenosiri. Kwa vile funguo za siri zinahifadhiwa katika Akaunti yako ya Google, zinapatikana kwenye vifaa vyako vyote vilivyosawazishwa.
-
Mbinu mpya za usalama wa akaunti
Kulingana na viwango vya FIDO Alliance na W3C, funguo za siri hutumia itifaki sawa za kriptografia za funguo za umma ambazo ndizo kiini cha funguo halisi za usalama, kwa hivyo haziwezi kuathiriwa na wizi wa data binafsi, matukio ya kuiba data binafsi kwenye shirika moja na kuzitumia kwenye shirika lingine na mashambulio mengine ya mtandaoni.
-
Njia salama zaidi ya kuingia katika akaunti kwenye huduma na programu unazopenda
Unastahili kupata kasi na usalama unapoingia katika akaunti zako zote za mtandaoni. Unaweza kuingia katika akaunti kwa usalama na urahisi zaidi kwenye maelfu ya programu na tovuti ukijua kwamba taarifa zako za kuingia katika akaunti zinahifadhiwa kwa faragha na usalama kwenye Akaunti yako ya Google.
Pata maelezo kuhusu jinsi ya kutumia kipengele cha 'Ingia ukitumia akaunti ya Google' -
Ingia katika akaunti au ujisajili kwa usalama mahali popote kwa kugusa tu
Kwa kujisajili na kuingia ukitumia akaunti ya Google, unalindwa dhidi ya watendaji wabaya wanaoweza kuiba manenosiri yako kwa niaba ya programu na huduma za wengine. Hata ikiwa programu au huduma ina tukio linalotishia usalama, kipengele cha kuingia ukitumia akaunti ya Google huendelea kukulinda kwa kuthibitisha kila hatua ya kuingia katika akaunti kwa njia ya kipekee.
-
Udhibiti zaidi wa akaunti na miunganisho yako
Dhibiti jinsi unavyotumia kipengele cha Kuingia ukitumia akaunti ya Google, akaunti zilizounganishwa na miunganisho mingine ya washirika wengine kwenye Akaunti yako ya Google. Unaweza kuangalia, kusasisha na kudhibiti data unayochagua kushiriki, vyote hivyo kwenye sehemu moja, hali inayohakikisha kuwa umepangilia vitu vyako na una udhibiti.
Kagua miunganisho yako sasa
-
Manenosiri thabiti husaidia kudumisha usalama wa data yako
Kuchagua manenosiri thabiti ya kipekee kwa ajili ya akaunti zako za mtandaoni ni hatua muhimu katika kudumisha faragha ya taarifa zako binafsi. Hata hivyo, watu wengi husema kuwa wanatumia nenosiri lile lile dhaifu kwenye tovuti nyingi, hali ambayo huongeza uwezekano wa kuathiriwa kwa usalama wa akaunti zao.
-
Kidhibiti cha Manenosiri cha Google hukusaidia kudhibiti funguo za siri na manenosiri yako
Dhibiti Funguo za siri na Manenosiri uliyohifadhiKidhibiti cha Manenosiri cha Google kilichojumuishwa kwenye Chrome na Android hupendekeza, huhifadhi na kujaza manenosiri kwa njia salama kwenye akaunti zako zote za mtandaoni. Funguo za siri hufanya kazi pamoja na manenosiri na hudhibitiwa kwa urahisi katika sehemu moja.
-
Vilinda Nenosiri vya kiotomatiki husaidia kulinda manenosiri yako
Kila siku, matukio mapya ya ufichuzi haramu wa data hufichua hadharani mamilioni ya majina ya watumiaji na manenosiri. Google hufuatilia ili kubaini manenosiri yaliyoathiriwa, kwa hivyo, iwapo mojawapo ya manenosiri uliyohifadhi limefichuliwa kwa njia haramu, tutakuarifu kiotomatiki.
Linda akaunti zako zote za mtandaoni kwa kufanya Ukaguzi wa Manenosiri. Pima uthabiti wa manenosiri yako, angalia iwapo umetumia nenosiri lolote zaidi ya mara moja na ufahamu iwapo kuna manenosiri yaliyoathiriwa.
kuimarisha usalama wako mtandaoni.
-
Vidhibiti vya faraghaChagua mipangilio ya faragha inayokufaa.
-
Kanuni za dataPata maelezo zaidi kuhusu jinsi tunavyoheshimu faragha yako kwa kutumia kanuni za data.
-
Vidokezo vya usalamaGundua vidokezo vya haraka na desturi bora za kuwa salama mtandaoni.
-
Matangazo na dataPata maelezo zaidi kuhusu matangazo unayoonyeshwa kwenye mifumo yetu.